Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, Dk Nkosazana Dlamini-Zuma , akizungumza katika Kikao cha kawaida cha 26 cha Baraza la Wakuu wa Nchi na Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia, Jumamosi na Jumapili iliyopita, alitoa wito kwa nchi zote za Afrika, kuona dharura ya kuwa na mipango ya haraka, kutekeleza yaliyokubalika katika prokali ya Kimataifa ya kukabiliana na mabadiliko hasi ya tabia nchi .
Licha ya kutambua kwamba, Afrika haichangii kwa kiwango kikubwa kimataifa , uharibu wa mazingira , bahati mbaya, ndilo bara linalo athirika vibaya zaidi na mabadiliko hayo . Hivyo ni lazima kupania kutekeleza hatua zote zinazoweza boresha hali ya hewa , ikiwemo kilimo safi na nishati mbadala, ili kuokoa maziwa, misitu, bahari na mito ya Afrika , na kupambana kwa uhakika zaidi dhidi ya majanga ya asili na hatari zingine za mabadiliko ya tabia nchi.
Mwenyekiti Dlamini, aliomba uwepo wa kasi katika dhamira mpya za utendaji barani Afrika, kuonyesha ukomavu baada ya kupita kipindi cha miaka 50, tangu kuundwa kwa AU, kwa lengo la kuwa na umoja katika kuleta mafanikio na amani na ustawi wa watu barani Afrika, wakisukumwa na kuongozwa na nguvu ya za wananchi. Na pia kama walivyokubalina katika ajenda za hadi mwaka 2063, katika kuleta mabadiliko mapya Afrika.
Alieleza na kuwasisitiza viongozi wenzake kwamba , ni kuanza sasa kuongeza kasi ya mageuzi kwa katika mwaka huu 2016, ambao ameutaja kuwa jukwaa la kuendeleza haki za binadamu kwa wakazi wote wa bara la Afrika katika utofauti wao wote. Na kwamba katika mwaka huu 2016, ambao umetajwa maalum kwa ajili ya utetezi wa Haki za Binadamu, ukilenga hasa kukuza haki za wanawake na wasichana, ni lazima kuongeza kasi ya mabadiliko. Ni lazima kuendelee kuweka watu wote na haki zao za msingi ,kama kituo kikuu rejea katika ajenda kufikia 2063.
Alikumbusha , ni pamoja na haki za watu kupata elimu, chakula na lishe, huduma za afya, huduma salama maji, usafi wa mazingira na nishati, maisha tulivu na amani, dhidi ya ukatili na msimamo mikali, haki ya uhuru wa kujieleza, uhuru wa vyombo vya habari na ulinzi dhidi ya ubaguzi wowote ule.
Pia alimewataka viongozi wa Afrika , kuhakikisha wanapima mambo kwa hekima kubwa kabla ya kutoa maamuzi yao katika hoja na matakwa ya watu wa Afrika, na katika kutatua matatizo ya Afrika , kwa manufaa ya sasa na kwa vizazi vijavyo.
All the contents on this site are copyrighted ©. |