2016-01-22 14:40:00

Dunia iko zaidi katika mwelekeo wa tiba za upasuaji


Tamko la pamoja lililotolewa katika Jukwaa la Mkutano wa Dunia wa Uchumi,wa hivi karibuni,Uswiss, Makampuni  ya Dawa zaidi ya 80, yamezitaka serikali kutengenza mkakati mpya wa kulipia gharama za kutengenza dawa za kupambana  na wadudu wabaya wanaoingia mwilini, dawa za antibiotics.

Katika tamko hilo makampuni hayo yameonyesha kujali kwamba,  thamani ya antibiotics, hailingani na  manufaa  yanayopatikana katika  jamii.  Hata hivyo, Makampuni  hayo yameahidi kuendelea kuwekeza katika tafiti na uboreshaji wa upatikanaji wa dawa za antibiotics duniani kote.   Kati ya makampuni hayo ni pamoja na makampuni mashuhuri kama  GSK, Merck, PFIZER na Johnson & Johnson.

Taarifa inaongeza,mara kwa mara  makampuni hayo, yamekuwa yakionya kwamba , dunia iko katika kingo za kushambuliwa vibaya na  vijidudu sugu, na hivyo ni lazima kuongeza bidii katika matarajio ya kupambana na maambukizi  ya maradhi yasiyotibika.  Na kwamba kuna mwelekeo mkubwa wa kuelemea katika tiba ya upasuaji  hasa kutokana na wingi wa  maradhi ya saratani na uwepo wa kitisho kikubwa cha matumizi ya dawa za antibiotics, kushindwa kufanyakazi kutokana na usugu wa vijidudu.

Kwa mujibu wa tamko hilo,  vijidudu sugu vinataweza ua watu milioni 10 kwa mwaka,  ifikapo mwaka 2050, na  kwamba itagharimu kiasi cha dola trilioni 100 katika katika pato la uchumi wa dunia, kutokana na mfumo wa sasa  wa kupambana na vijidudu  kuonekana kwa kiasi kikubwa kushindwa, licha ya uwekezaji wa mabilioni ya dola. Hivyo ni lazima kuwe na njia mpya  zinazoweza kutoa msaada katika juhudi za  uvumbuzi na ugunduzi wa madawa yanayoweza kufanikisha tiba dhidi ya mashabulio la vijidudu sugu.  Ni msisitizo uliomo katika tamko la  makampuni 85 ya madawa kwa serikali, kutoa msaada wa kutosha kwa ajili ya ugunduzi na utengenzaji wa dawa mpya za antibiotics na pia katika kutengeneza maendeleo endelevu nautabiri wa soko kwa dawa mpya. 








All the contents on this site are copyrighted ©.