2016-01-21 10:25:00

Balozi Robert Compaore wa Burkina Faso awasilisha hati zake za utambulisho!


Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi, tarehe 21 Januari 2016 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Bwana Robert Compaore, Balozi mpya wa Burkina Faso mjini Vatican. Balozi Compaore alizaliwa kunako tarehe 4 Oktoba 1965 na tangu mwaka 1988 amefanya kazi sehemu mbali mbali kama mfanyakazi wizarani; Katibu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa; Katibu Ubalozi wa Burkina Faso nchini Ufaransa; Mshauri wa mambo ya nchi za nje hadi kufikia mwaka 2004.

Balozi Compaore kuanzia mwaka 2004 hadi mwaka 2006 alikuwa ni kiongozi mkuu idara ya ushauri wa kisheria. Baadaye aliteuliwa kuwa Mkurugenzi mkuu wa rasilimali watu; mshauri wa pili katika Ubalozi wa Burkina Faso nchini Ubelgiji; mshauri wa masuala ya mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa. Baadaye aliteuliwa kuwa ni mshauri mkuu wa mambo ya kisiasa na kidiplomasia kwa Mwenyekiti wa Tume ya CEDAO huko Guinea Bissau. Na katika mwaka 2013 akateuliwa kuwa mshauri wa kisiasa na kidiplomasia huko ECOMIB.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.