2016-01-16 13:51:00

Askofu mkuu Pezzuto ateuliwa kuwa Balozi mpya wa Vatican kwenye Ufalme wa Monaco


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Luigi Pezzuto kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Monaco, kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Pezzuto alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Bosnia, Erzegovina na Montenegro. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Pezzuto alizaliwa kunako tarehe 30 Aprili 1946 huko Squinzano, Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, akapewa Daraja Takatifu la Upadre hapo tarehe 27 Septemba 1971.

Tarehe 6 Januari 1997 akateuliwa na Mtakatifu Yohane Paulo II kuwa Askofu mkuu. Tangu wakati huo amekwisha tekeleza dhamana na utume wake wa kidiplomasia nchini DRC, Gabon, Tanzania, El Salvador, Beliza, Antilles na mwishoni aliteuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Bosnia-Herzegovina na Montenegro.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.