2016-01-14 14:39:00

Mh. Padre Euzebius C. O. Managwu, ateuliwa kuwa Askofu wa Jimbo la Port-Gentil


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa sana Padre Euzebius Chinekezy Ogbonna Managwu kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Port-Gentil, nchini Gabon. Kabla ya utuezi huu, Askofu mteule Ogbonna Managwu alikuwa ni Makamu Askofu Jimbo kuu la Libreville, Gabon. Askofu mteule Managwu alizaliwa tarehe 13 Desemba 1959, mjini N’Djamena, Chad na wazazi kutoka Nigeria, waliohamia nchini Gabon. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, kunako tarehe 1 Novemba 1992 akapewa Daraja Takatifu la Upadre, Jimbo kuu la Libreville. Tangu wakati huo, amekuwa ni Paroko Msaidizi, Paroko, Padre mshauri wa kiroho Seminari ndogo ya Saint Jean, Libreville; Makamu Askofu Jimbo kuu la Libreville; Mlezi na kuanzia mwaka 2006 hadi mwaka 2010 alikuwa ni Paroko na Dekano wa Libreville ya Kusini.

Mwaka 2010 hadi kuteuliwa kwake kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki Port-Gentil alikuwa ni Makamu Askofu Jimbo kuu la Libreville, Gabon. Jimbo la Port-Gentil, Gabon limekuwa wazi tangu mwaka 2013 baada ya Askofu Mathieu Madega Lebouakehan kuhamishiwa Jimbo Katoliki la Mouila, Gabon.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.