2016-01-04 07:16:00

Mh. Padre Cèlestin-Marie Gaoua ateuliwa kuwa Askofu wa Jimbo la Sokodè, Togo


Baba Mtakatifu Francisko amekubali ombi la kung’atuka kutoka madarakani lililowasilishwa kwake na Askofu Ambroise Kotamba Djoliba wa Jimbo Katoliki Sokodè kadiri ya Sheria za Kanisa namba 401§ Ibara ya 1.Wakati huo huo, Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Mheshimiwa Padre Cèlestin-Marie Gaoua, Gombera wa wa Seminari kuu ya Falsafa ya Tchitchao, iliyoko Jimbo Katoliki la Kara, Togo kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki Sokodè, Togo.

Askofu mteule Cèlestin-Marie Gaoua alizaliwa tarehe 6 Aprili 1957. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, kunako tarehe 27 Desemba 1986 akapewa Daraja takatifu la Upadre. Tangu wakati huo, katika maisha na utume wa Kipadre amebahatika kuwa: Gombera kuanzia mwaka 1987 hadi mwaka 1994. Kati ya mwaka 1994 hadi mwaka 1999 alikwenda nchini Ufaransa kwa ajili ya masomo ya juu.

Kuanzia mwaka 2000 hadi mwaka 2009 alikuwa ni Padre Mmissionari wa Fidei Donum Jimboni Sokodè. Baadaye ajateuliwa kuwa Paroko na Msimamizi wa Parokia ya Notre dame mjini Kulunde. Kuanzia mwaka 2009 hadi mwaka 2015 alikuwa ni Gombera wa Seminari kuu ya falsafa ya Benedikto XVI iliyoko Tchiutchao, Jimbo Katoliki la Kara, Togo.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.