2015-12-31 15:43:00

Makatibu wakuu wapya serikali ya awamu ya tano Tanzania


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu katika Wizara kumi na nane zinazounda Serikali ya awamu ya tano!

Walioteuliwa ni kama ifuatavyo;

Katibu Mkuu Kiongozi: Balozi - Ombeni Sefue

Katibu Mkuu Ikulu: Peter Ilomo

Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora Dkt. Laurian Ndumbaro

Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)

Mhandisi Mussa Iyombe (Katibu Mkuu)

Dkt. Deo Mtasiwa (Naibu Katibu Mkuu - Afya)

Bernard Makali (Naibu Katibu Mkuu - Elimu)

Ofisi ya Makamu wa Rais

Mbaraka A. Wakili ( Katibu Mkuu)

Mhandisi Ngosi Mwihava (Naibu Katibu Mkuu)

Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge, Sera, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu)

Erick Shitindi (Katibu Mkuu Kazi na Ajira)

Mussa Uledi (Katibu Mkuu Bunge)

Dkt. Hamis Mwinyimvua (Katibu Mkuu - Sera)

Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi

Dkt. Frolence Turuka (Katibu Mkuu - Kilimo)

Dkt. Mashingo (Katibu Mkuu Mifugo)

Dkt. Budeba (Katibu Mkuu - Uvuvi)
 

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Mhandisi Joseph. Nyamuhanga (Katibu Mkuu - Ujenzi)

Dkt. Leonard M. Chamuliho (Katibu Mkuu - Uchukuzi)

Profesa Faustine R. Kamuzora (Katibu Mkuu - Mawasiliano)

Mary Sassabo (Naibu Katibu Mkuu Mawasiliano)

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Dkt. Yamungu Kayandabira (Katibu Mkuu)

Dkt. Moses Kusiluka (Naibu Katibu Mkuu)

Wizara ya Maliasili na Utalii

Meja Jenerali Gaudence S. Milanzi (Katibu Mkuu)

Anjelina Madete (Naibu Katibu Mkuu)

Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji

Dkt. Adelhem James Meru (Katibu Mkuu - Viwanda)

Profesa Adolf F. Mkenda (Katibu Mkuu - Biashara na Uwekezaji)

Mhandisi Joel Malongo (Naibu Katibu Mkuu)
 

Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.

Maimuna Tarishi (Katibu Mkuu)

Profesa Simon S. Msanjila (Naibu Katibu Mkuu)

Dkt. Leonard Akwilapo (Naibu Katibu Mkuu)

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

Dkt. Mpoki Ulisubisya (Katibu Mkuu - Afya)

Sihaba Nkinga (Katibu Mkuu - Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto)

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

Profesa Elisante Ole Gabriel Mollel (Katibu Mkuu)

Nuru Halfan Mrisho (Naibu Katibu Mkuu)

Wizara ya Maji na Umwagiliaji

Mhandisi Mbogo Futakamba (Katibu Mkuu)

Mhandisi Kalobero Emmanuel (Naibu Katibu Mkuu)

Wizara ya Nishati na Madini

Profesa Justus W. Ntalikwa (Katibu Mkuu)

Profesa James Epifani Mdoe (Naibu Katibu Mkuu)

Dkt. Paulina Pallangyo (Naibu Katibu Mkuu)

Wizara ya Katiba na Sheria

Profesa Sifuni Mchome (Katibu Mkuu)

Suzan Paul Mlawi (Naibu Katibu Mkuu)

Amon Mpanju (Naibu Katibu Mkuu)

Wizara ya Mambo ya Ndani

Jaji Meja Jenerali Projest A. Rwegasira (Katibu Mkuu)

Balozi Hassan Simba Yahaya (Naibu Katibu Mkuu)
 

Wizara ya Fedha na Mipango

Dkt. Silvacius Likwelile (Katibu Mkuu)

Dorothy Mwanyika (Naibu Katibu Mkuu)

James Dotto (Naibu Katibu Mkuu)

Amina Hamis Shaban (Naibu Katibu Mkuu)

Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa

Dkt. Aziz Mlima (Katibu Mkuu)

Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi ( Naibu Katibu Mkuu)


Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

Job D. Masima (Katibu Mkuu

Immaculate Peter Ngwale (Naibu Katibu Mkuu.

Makatibu wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wote ambao hawajatajwa katika orodha hii watapangiwa kazi nyingine. Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Eliakimu Maswi kuwa Kaimu Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na ametengua uteuzi wa Naibu Kamishina wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Lusekelo Mwaseba, ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Ikulu, Dar es Salaam.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.