2015-12-24 09:08:00

Mama Theresa wa Calcutta kutangazwa kuwa Mtakatifu!


Kardinali Angelo Amato, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la kuwatangaza waamini kuwa wenyeheri na watakatifu baada ya kukutana na kuzungumza na Baba Mtakatifu Francisko hivi karibuni, ameridhia kwamba, Mama Theresa wa Calcutta, Mwanzilishi wa Shirika la Wamissionari wa Upendo atangazwe kuwa ni Mtakatifu, katika tarehe itakayopangwa baada ya Mkutano wa Makardinali. Mama Theresa wa Calcutta anatangazwa wakati huu Mama Kanisa anapoadhimisha Mwaka Mtakatifu wa Jubilei ya huruma ya Mungu sanjari na Mwaka wa Watawa Duniani.

Tarehe rasmi itajulikana mara baada ya mkutano wa Makardinali, lakini wachunguzi wa mambo wanasema, pengine itakuwa ni tarehe 4 Septemba 2016, tukio ambalo litanatarajiwa kuwavuta watu wengi kutoka sehemu mbali mbali za dunia ili kushiriki, kwani Mama Theresa wa Calcutta, amekuwa ni mama wa maskini na wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii! Katika maisha na utume wake, akawapatia kipaumbele cha pekee kwa kuitambua ile sura ya huruma ya Mungu. Mama Theresa wa Calcutta alijipatia nguvu za kuweza kutekeleza utume huu mgumu kati ya maskini kutoka katika maadhimisho ya Fumbo la Ekaristi Takatifu na Ibada kwa Ekaristi Takatifu.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.