2015-12-24 17:06:00

Kadi ya Salam za Noeli kutoka kwa Papa Francisko


Kama ilivyo kawaida wakati wa Siku kuu kama hizi, watu kutumiana kadi za salam na matashi mema ya Siku kuu ya Noeli na Mwaka mpya, 2016, Baba Mtakatifu Francisko katika kadi yake ya salam za Noeli anasema kwa lugha ya Kilatini kwamba, “Exultemus in die salutis nostrae” Tushangilie siku hii ya wokovu wetu! Haya ni maneno yaliyotolewa kwenye mahubiri ya Mtakatifu Leo mkuu na kuyatumia kwa ajili ya salam na matashi mema kwa ajili ya Sherehe ya Noeli kwa Mwaka 2015.

 Kadi hii inaonesha pia picha ya Mtoto Yesu anayeabudiwa na Malaika, iliyochorwa na Carlo Maratta, aliyezaliwa kunako mwaka 1625 huko Ancona, Italia. Huyu ni kati ya wachoraji mahiri nchini Italia. Na kwa kadi hii, Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican inapenda pia kukutakia kila la kheri na Baraka kwa Sherehe ya Noel ina mwendelezo mwema wa maadhimisho ya Mwaka Mtakatifu wa Jubilei ya huruma ya Mungu.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.