2015-12-23 17:07:00

Tanzania na Rwanda kuendeleza ushirikiano katika nyanja mbali mbali!


Uswiss imeahidi kuendeleza ushirikiano na Tanzania  Katika nyanja mbalimbali za maendeleo huku mkazo mkubwa ukiuelekeza katika kuendeleza elimu ya mafunzo ya ufundi stadi. Balozi wa Uswisd nchini Tanzania Mheshimiwa Florence Tinguelly Mattli, amesema hayo tarehe 23 Desemba, 2015 alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu Jijini Dar es Salaam. Balozi Florence amemueleza Rais Magufuli kuwa pamoja na kuwepo kwa miradi mingine ambayo nchi hiyo ina endelea kuitekeleza kwa kushirikiana na Tanzania, katika awamu hii Uswiss itatilia mkazo katika elimu ya ufundi stadi ili kuwawezesha vijana wanaosoma kuwa na ujuzi unaowawezesha kuzalisha bidhaa na kujipatia kipato kama ambavyo nchi ya Uswiss inafanya.

Maeneo mengine ambayo viongozi hao wamezungumzia ni kuimarisha ushirikiano katika uwekezaji, ambapo Rais Magufuli amewaalika wawekezaji kutoka Uswiss kufanya biashara na Tanzania, kuimarisha huduma za bandari na pia kuongeza uwezo katika kukabiliana na vitendo vya Rushwa. Kuhusu Sekta ya afya, Rais Magufuli ameipongeza Uswiss kwakushirikiana na Tanzania kupitia Taasisi ya Afya Ifakara katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiafya ikiwemo kukabiliana na ugonjwa wa Malaria na ameahidi kuwa Serikali itaendelea kuitumia taasisi hiyo ili kusaidia juhudi za kukabilianana magonjwa.

Wakati HuoHuo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mheshimiwa Jasem Al NajemIkulu, Jijini Dar es salaam. Katika Mazungumzo hayo, Balozi Al Najem amewasilisha salamu za Mfalme wa Kuwait Mheshimiwa Sabah Al Ahamad Al Jaber al Sabah kwa Rais Magufuli, ambaye amempongeza kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano na amemhakikishia kuwa Kuwait itaendelea kushirikianana Tanzania katika maendeleo ikiwemo kufadhili utekelezaji wa miradi mbalimbali katika    sekta za ujenzi, Maji na Kilimo.

Miongoni mwa miradi hiyo ni mradi wa ujenzi wa barabara ya Chaya – Nyahua yenye urefu wakilometa 85 kwa kiwango cha lami ambapo Tanzania imeomba ufadhili wa dola milioni 85, Mrad iwa Majiwa Same - Mwanga – Korogwe ambapo Tanzania imeomba ufadhili wa dola milioni 20 na Mradi mkubwa wa kilimo cha umwagiliaji katika bonde la Mhongo na Luhiche Mkoani Kigoma ambapo Kuwait imeonesha nia ya kuufadhili. Aidha, Rais Magufuli amemshukuru Mfalme wa Kuwait kwa salamu zake za pongezi na amewaalika wafanyabiashara wa Kuwait kushirikiana na Tanzania katika biashara na uwekezaji.

Katika Hatua nyingine, Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekutananaWaziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Mheshimiwa Louise Mushikiwabo aliyetumwa kuleta ujumbe maalum wa Rais Paul Kagame wa Rwanda. Katika Ujumbe huo, Mheshimiwa Kagame amemhakikishia Rais Magufuli kuwa Rwanda itaendelea kushirikianana Tanzania katika nyanja mbalimbali za kiuchumi, kisiasa na kijamii hasa ikizingatiwa kuwa licha ya kuwa ni nchi jirani ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Rwanda  ni marafiki na nduguwa Tanzania.

Rais Kagame pia amempongeza RaisMagufuli kwa uongozi mzuri aliounesha katika siku za mwanzo za uongozi wake wa awamu ya tano ambao amesema anauunga mkono. Pamoja na kupokea salamu za Rais Kagame, Rais Magufuli na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda wamezungumzia mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini Burundi na wote kwa pamoja wameona ni muhimu kupata suluhisho kwa njia ya mazungumzo ili wananchi waweze kuishi kwa amani na kuendelea na shughuli zao  za maendeleo.

Na mwandishi maalum.

Dar es Salaam.








All the contents on this site are copyrighted ©.