2015-12-21 16:09:00

Vigogo wa mawasiliano wateuliwa mjini Vatican!


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Bwana Stefano D’Agostini kuwa Mkurugenzi mpya wa Kituo cha Televisheni cha Vatican, CTV na ataendelea kuwa ni mhusika mkuuwa shughuli za kiufundi za Kituo cha Televisheni cha Vatican ambacho ni msaada mkubwa katika kurusha matukio mbali mbali ya Kanisa kitaifa na kimataifa.

Wakati huo huo, Baba Mtakatifu amemteua Dokta Greg Burke kuwa Msemaji mkuu msaidizi wa Vatican, wajibu ambao utaanza kutekelezwa hapo tareh Mosi, Februari 2016. Kabla ya uteuzi huu alikuwa ni mshauri wa masuala ya mawasiliano katika kitengo cha huduma za kawaida Sekretarieti ya Vatican.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.