2015-12-15 14:15:00

Papa : Kutumaini huruma ya Mungu hutuweka Huru


Baba Mtakatifu Jumatatu, aliwatia moyo waamini  akiwataka waishi kwa kutumiani huruma ya Mungu kwa kuwa hufungua milango ya upeo na humfanya mtu kuona mbali na kuwa huru dhidiya wasiwasi, mashaka, woga na kutenda dhambi. Baba Mtakatifu  aliasa wakati wa homilia yake  mapema Jumatatu , akiwa katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta la hapa Vatican.  Tafakari ya Papa ilimtazama Balaamu aliyetajwa katika Somo la Kwanza kutoka Kitabu cha Hesabu,  nabii aliyekodishwa na  mfalme kuilaani Israeli, licha ya Balaamu kuwa na makosa na dhambi pia, kama tulivyo pia sisi sote,watu wenye makosa na dhambi bado Mungu anatutaka kuwa wajumbe wake. 

Papa alisema  hakuna sababu za kuwa na hofu au woga katika kuomba  msamaha kwa dhambi zetu , kwa kuwa Mungu wetu ni Mungu Mkuu mwenye kuziona dhambi zetu na hutusamehe kila tunapoomba kusamehewa. Binadamu anapaswa kutambua kwamba, Mungu ni mkuu kuliko dhambi zetu. Kama ilivyokuwa kwa Baalamu alipokutana na Malaika wa Bwana , alifanya mabadiliko ndani ya moyo wake, na ndivyo nasi pia tunapokutana na Bwana katika Sakramenti ya Kitubio ni tunapaswa kubadilika kiroho. Ni wakati wa kuanza kuona kile tulichokosea, kuuona  ukweli ,  kama ilivyokuwa kwa Balaamu alivyowaona  watu wa  Mungu  wanaoishi katika katika mahema katika jangwa na zaidi ya jangwa  kukiwa na mafanikio ya, uzuri na ushindi.

Balaamu aliufungua moyo wake na kutubu. Aliuona ukweli kwamba matendo mema na huruma kwa wengine daima huonyesha  ukweli , Ukweli wenye kuwa na matumaini. Na hivyo matumaini hayo kwa Mkristo inakuwa ni fadhila , ambayo ni zawadi kuu kutoka kwa Mungu,  zawadi yenye kuturuhusu kuona  zaidi ya matatizo na matesna hasa  zaidi sana yanayotokana dhambi zetu.  Ni Matumaini yenye kuturuhusu  sisi kuona uzuri wa Mungu. Pia kwamba,  kwa wale wenye kuwa na fadhila hii ya matumaini, pia huwa huru na nguvu za kuona mbele zaidi ya mabaya ya  nyakati, iwe kwa ajili ya afya yao au kwa ajili ya familia yao.

Aidha Baba Mtakatifu akitafakari juu ya somo la Injili ambamo Makuhani Wakuu walimwuliza Yesu ni kwa mamlaka gani anatenda, anawaona makuhani hao kuwa hawakuwa na upeo wa kuona mbali, walikuwa ni watu waliojifungia katika uelewa wao  wa kibindamu , mioyo yao ilikuwa migumu kujifunua wazi kwa Bwana wa Ukweli na matumaini.  Papa anataja hoja za kibinadamu kwamba  huifunga mioyo , hufungia nje uhuru wa kuelewa yaliyo ya juu , hufungia nje matumaini  yenye kutufanya kutuweka huru dhidi ya dhambi.

Papa Francisko aliendelea kuzungumzia juu ya uzuri wa uhuru,  matumaini ya wanaume na wanawake wa Kanisa. Na pia aligusia upande wa pili wa mioyo migumu ya wanaume na wanawake wa Kanisa ambao wamejifungia katika hoja zao, wakikataa kufanya mabadiliko moyoni na hivyo kuwa watu wasioona ukweli na wala kuwa na matumaini mapya yenye kuwapa uhuru kamili.

Alieleza hayo na kutoa wito kwamba, katika  mwaka huu wa  kuomba Huruma ya Mungu , mna njia mbili kuu, moja ni ile  ya wale wenye kuwa na  matumaini katika huruma ya Mungu, wenye  kutambua kwamba,  Mungu ni Baba na njia ya pili ni wale ambao hawataki mageuzi ya kiroho, watu walioshikilia ya kale yanayowafanya kuwa watumwa wa dhambi,  ambao hawataki kujua lolote juu ya huruma ya Mungu.

Papa Francisko, alihitimisha hotuba yake kwa kukumbuka tukio la Buenos Aires mwaka 1992, wakati wa Ibada ya Misa kwa wagonjwa, ambamo aliutumia muda mrefu kuungamisha na mwanamke mkongwe alimwendea macho yake yakiwa yamejawa na matumaini na kumwambia  nimekuja ungama kwa sababu sisi sote ni wadhambi . Na kama Mungu hatusamehi dunia isingekuwepo. Papa alivutiwa na maneno ya mkongwe huyo. Amesema  ndivyo ilivyo katika maisha yetu ya kila siku, kuna wale wenye kumtumaini huruma ya Mungu  na wale waliosadiki katika matumaini hayo, walio ifunga mioyo yao wenyewe katika utumwa wa dhambi . Lakini tunapaswa kukumbuka maneno ya  mwanamke Mkongwe na Injili kwamba , Mungu  husaheme yote, na daima anasubiri tutubu dhambi zetu ili tupate kuwa karibu Nae na hivyo kuwa huru  dhidi ya mateso ya dhambi. 








All the contents on this site are copyrighted ©.