2015-12-14 15:45:00

Papa akutana na Rais wa Jamhuri ya Sri Lanka


Mapema Jumatatu hii , Baba Mtakatifu Francisko, alimpokea na kuwa na mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Sri Lanka, Mheshimwa Rais Maithripala Sirisena akiw aameandamana na mkewe.

Baada ya kukutana na Papa Francisko , Rais Sirisena, alikutana na Katibu wa Vatican,   Kardinali Pietro Parolin. Majadiliano ya viongozi hawa yalifanyika katika hali ya  urafiki na maelewano,maongezi  yakitwaliwa na  kumbukumbu  ziara ya Papa  ya mwezi Januari mwaka huu barani Asia.  Aidha walizungumzia  baadhi ya masuala ya nchi  ya Sri Lanka, hasa juu ya mchakato wa amani na maridhiano katika maendeleo, katika matazamio na matumaini ya kukuza nguvu ya maelewano  kijamii . Na pia walizungumzia  mchango wa Kanisa Katoliki katika sekta mbalimbali za jamii na umuhimu wauwepo wa mazungumzo baina ya dini.  Na walibadilishana mawazo juu ya mazingira hasa wakielekeza katika matokeo ya Mkutano wa Paris juu ya Mabadiliko ya tabianchi, mkutano  muhimu wa kimataifa, uliokamilika hivi karibuni. 








All the contents on this site are copyrighted ©.