2015-12-10 15:29:00

Kanisa limempoteza mwanadiplomasia, Kard. Carlo Furno!


Kardinali Carlo Furno, aliyekuwa mhudumu mkuu wa Kanisa kuu la Bikira Maria mkuu mjini Roma amefariki dunia hapo tarehe 9 Desemba 2015 akiwa na umri wa miaka 94. Alizaliwa kunako mwaka 1921. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi akapadrishwa kunako mwaka 1944, wakati ambapo vita kuu ya Pili ya Dunia ilikuwa imepamba moto duniani! Kwa miaka mingi alitoa huduma yake ya kichungaji kwenye diplomasia ya Vatican.

Kunako mwaka 1973 akateuliwa kuwa Askofu mkuu na Balozi wa Vatican nchini PerĂ¹. Baadaye alihamishiwa Lebanon na Italia. Kunako mwaka 1995 hadi mwaka 2007 aliteuliwa kuwa Mkuu wa Shirika la kulinda Kaburi Takatifu Yerusalemu. Baadaye aliteuliwa kuwa mwakilishi wa kitume kwenye Makanisa makuu ya Mtakatifu Francisko na baadaye, Kanisa kuu la Bikira Maria mkuu, lililoko mjini Roma. Kunako mwaka 1994 Papa Yohane Paulo II akamteuwa kuwa Kardinali.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.