2015-12-10 15:54:00

Hija za kichungaji za Papa Francisko nchini Italia zimefutwa kwa sasa!


Kardinali Angelo Scola, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Milano, Italia, Alhamisi, tarehe 10 Desemba 2015 amewaambia waandishi wa habari kwamba, hija ya kichungaji ya Baba Mtakatifu Francisko Jimbo kuu la Milano, iliyokuwa ifanyike tarehe 17 Mei 2016 imehairishwa hadi mwaka 2017. Baba Mtakatifu Francisko ameamua kufuta hija zote za kichungaji nchini Italia wakati wote wa maadhimisho ya Mwaka Mtakatifu wa Jubilei ya huruma ya Mungu kutokana na ratiba kubana sana! Kardinali Scola anasema Baba Mtakatifu akipata nafasi katika kipindi hicho, basi atawatembelea Jimbo kuu la Milano!

 

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.