2015-12-07 08:15:00

Kampuni ya PwC yateuliwa kuwa ni mkaguzi wa nje wa fedha ya Vatican


Baraza la Kipapa la Uchumi katika kikao chake cha hivi karibuni kwa kupata baraka kutoka kwa Baba Mtakatifu Francisko aliyewapongeza kwa hatua kubwa waliyokwisha fikia katika mchakato wa mageuzi katika masuala ya fedha, uchumi na uongozi mjini Vatican, Baraza hili limepiga hatua kubwa zaidi. Kwa sasa limechagua kampuni mpya ya wakaguzi wa hesabu za Vatican.

Wachunguzi wa mambo wanasema, hii ni kati ya Kampuni muhimu sana katika masuala ya ukaguzi wa fedha kimataifa. Baraza hili limeridhia ushauri uliotolewa na Kamati ya usimamizi wa fedha kwa kuridhia utendaji wa kampuni ya “Pricewaterhousecoopers” “PwC”. Kampuni hii itashirikiana na Baraza la Kipapa la uchumi katika ukaguzi wa mahesabu ya Vatican kwa kuzingatia ukweli na uwazi; ufanisi na tija, ili fedha ya Kanisa iweze kutumika kadiri ya malengo yake, yaani kusaidia mchakato wa Uinjilishaji wa kina kwa kuzingatia mahitaji ya mtu mzima: kiroho na kimwili.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican. 








All the contents on this site are copyrighted ©.