2015-12-07 15:52:00

Balozi Eduard Habsburg wa Hungaria awasilisha hati zake za utambulisho


Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 7 Desemba 2015 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Balozi Eduard Habsburg- Lothringen wa Hungaria mjini Vatican. Balozi Lothringen alizaliwa tarehe 12 Januari 1967, ameoa na ana watoto sita. Kunako mwaka 1995 alijipatia shahada ya uzamivu katika masuala ya falsafa.

Katika maisha yake Balozi Eduard Habsburg-Lothringen amejikita zaidi katika sekta ya filamu; akawa msemaji mkuu wa Askofu Klaus Kùng wa Jimbo Katoliki la Mtakatifu Polten. Amewahi kuwa mcheza picha na mwandishi wa Vituo mbali mbali vya Televisheni na Mratibu mkuu wa shughuli za mawasiliano katika familia ya Habsburg.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.