Jumatatu 30 Novemba, Kardinali Pietro Parolini, alitoa mchango wa Jimbo la Papa, kwa niaba ya Papa Francisko , katika Mkutano wa Viongozi wa Dunia unaotafuta kuweka makubaliano mapya kwa ajili ya kusalimisha dunia dhidi ya mabadiliko mabaya ya tabia nchi na hali ya hewa. Mkutano huo wa COP-21, uliosubiriwa kwa muda mrefu, unafanyika Paris Ufaransa, kama hatua inayofuatia kukamilika kwa makubaliano ya Kyoto yaliyomaliza muda wake mwaka huu .
Jimbo la Papa limetoa mchango wake kwa matumani makubwa kwamba, Mkataba Mpya wa Kimataifa juu ya mabadiliko ya tabia nchi , utapitishwa kwa kuzingatia kanuni za umoja na mshikamano kwa ajili ya utendaji wa haki, usawa na ushirikiano katika kufanikisha malengo makuu matatu, ambayo ni kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya hewa, kupambana na umaskini, na kukukuza hadhi na ustawi wa binadamu wote, kwa kizazi cha sasa na vijavyo baadaye. .
Hivyo Jimbo la Papa linaomba Makubaliano haya mapya ya kimataifa, yawezeleta mabadiliko ya lazima kupitia mihimili ya nguzo kuu tatu. Kwanza ni nguzo inayoshikilia mwelekeo wazi wa kimaadili, katika msukumo wa nia na madhumuni ya utekelezaji wa yatakayoandikwa katika Mkataba, kwa utambuzi kwamba, wanaoishi katika mazingira magumu na wanaopambana na athari za uzushi wa mabadiliko ya tabia nchi, ni watu maskini na pia vizazi vya baadaye ambavyo vinaweza kabiliwa na madhara makubwa zaidi, iwapo binadamu wa sasa hataonyesha kujali matokeo ya utendaji wake kwa sasa kwa siku za baadaye, kama wajibu wake. Hivyo katika utambuzi huo, Jimbo la Papa linahimiza wajibu wa kimaadili katika kuchukua hatua za utendaji wenye kulinda na kutetea mazingira, kwa mshikamano wa kimataifa, kama wajibu wa kawaida, kulingana na uwezo na masharti yatakayowekwa na wote..
Nguzo ya pili inahusiana na ukweli kwamba, Mkataba haipaswi tu kuangalia njia za kutekeleza hayo, lakini pia juu ya yote, kusambaza kanuni na ishara wazi zenye kuongoza mwenendo wa watendaji wote muhimu si tu kwa serikali kuu lakini pia serikali za mitaa, dunia biashara, jamii ya kisayansi na asasi za kiraia. Katika mtazamo huu, nchi zenye rasilimali nyingi zaidi nazenye uwezo zinapaswa kuongoza na kuwa mfano,katika haja ya kukuza sera na mipango ya maendeleo na uchumi endelevu.
Nguzo tatu, ni katika mwendelezo wa mazuri yote hata kwa siku za baadaye, na hivyo makubaliano haya ya COP-21, lisiwe tukio la kutia nanga majadiliano hayo lakini ni iwe ni mwanzo wa mchakato huu muhimu , katika ujenzi wa makubaliano thabiti zaidi ya pamoja, kupitia taratibu za kuiziishi ahadi na ufuatilia wake kwa uwazi, ufanisi na nguvu zaidi katika kuchukua hatua kwa ajili ya kuongeza kiwango cha hamu ya kuhakikisha udhibiti sahihi wa hali ya hewa na mabadiliko ya tabia nchi. Pia, ni lazima kufikiria utekelezaji kwa ajili ya uzalishaji endelevu, matumizi na mitazamo mipya katika maisha ya kijamii. Na hapo inakuwa ni kuzama katika misingi muhimu ya ufunguo wa elimu na mafunzo,ambavyo kwa bahati mbaya, wakati mwingine, huishia katika meza za mazungumzo ya mikataba ya kimataifa. Jimbo la Papa limesema, ufumbuzi wa kiufundi ni muhimu, na haitoshi kama haiwezekani kuingiza haki ya elimu, kwa ajili ya maisha endelevu na uelewa katika uwajibikaji. Jimbo la Papa limehimiza njia ya maisha ya sasa , pamoja na utamaduni wake wa taka ambao si endelevu, ni lazima kupata mbadala kwa njia ya elimu na maendeleo endelevu. Jimbo laPapa limetaja hilo kuwa ni Changamoto kubwa kitamaduni, kiroho na kielimu.
Kardinali alikamilisha maelezo yake kwa kutaja matumaini ya Papa Francisco juu ya mkutano huu kwamba, utaweza kukamilika kwa kupitisha Mkataba imara wa kimataifa, unaoweza leta mabadiliko mapya na wazi, katika mwelekeo wa kimaadili, wenye kuonyesha ishara thabiti kwa wadau wote, kupitisha maono thabiti katika Mkataba wa muda mrefu, kwa ajili ya ufanikishaji wa malengo matatu , ambayo ni kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya hewa, kupambana na umaskini, kudumisha heshima ya binadamu.
All the contents on this site are copyrighted ©. |