2015-11-28 08:14:00

Papa Barani Afrika: Kenya wamefunika, Uganda wanataka kuonesha makali yao!


Baba Mtakatifu Francisko akiwa njiani kuelekea Uganda katika hija yake ya kitume amemtumia Rais Uhuru Kenyatta salam na matashi mema, lakini zaidi kwa kumshukuru na kumpongeza kwa makaribisho makubwa ambayo amepokea kutoka kwa Familia ya Mungu nchini Kenya. Baba Mtakatifu anapenda kuwahakikishia wananchi wote wa Kenya mshikamano kwa njia ya sala pamoja na kuwapatia baraka zake za kitume, ili kweli Kenya iweze kuwa na baraka ya amani, nguvu na maendeleo.

Baba Mtakatifu alipoingia kwenye anga la Uganda, hata kabla ya kukutana na Rais Yoweri Kaguta Museveni, alimtumia salam za matashi mema pamoja na wananchi wote wa Uganda na kwamba anafurahia kujisikia nyumbani kati ya wananchi wa Uganda na hivyo anawatakia wananchi wote wa Uganda baraka zake za kitume!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.