2015-11-28 12:24:00

Askofu mwandamizi Jean Salomon Lezoutiè ateuliwa kuwa Askofu wa Yapougon


Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi la Askofu Laurent Akran Mandjo la kung’atuka katika uongozi wa Jimbo Katoliki la Yopougon, Pwani ya Pembe kadiri ya Sheria za Kanisa namba 401 Ibara ya 1. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu amemteua Askofu mwandamizi Jean Salomon Lezoutiè wa Jimbo Katoliki la Yopougon kuwa Askofu mpya wa jimbo hili.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.