Wakatoliki na Walutheri wametakiwa kuomba msamaha na kusameheana kati yao kwa ajili ya kashfa ya mgawanyiko wa siku za nyuma, hasa kwa wakati huu wanapo tembea pamoja katika utumishi wa maskini na wahitaji. Ilikuwa ni kiini cha ujumbe wa Papa alioutoa siku ya Jumapili iliyopita, wakati alipotembelewa na Viongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri la Roma, kwa ajili ya kuwa na Ibada ya sala ya jioni kwa pamoja. .
Baada ya kujibu maswali kadhaa yaliyoulizwa na wageni wake , kutoka jumuiya ya Kilutheri ya Roma , Papa Francisco alizungumzia jinsi Yesu kiongozi wao wote, anavyowaongoza katika njia ya kutembea pamoja kwa upendo kupitia huduma mbalimbali kwa maskini katika moyo wa maisha ya Kanisa na huduma.
Hotuba ya Papa alikumbuka adha na madhulumu ya siku za nyuma yaliyofanywa na Wakatoliki na Walutheri, dhidi ya kila mmoja , akisema kwamba leo ni lazima kuomba msamaha na kuchagua kutumikia pamoja, kama vile Yesu alivyoamuru kutumikiana mmoja kwa mwingine kwa upendo na umoja kamili” Baba naomba hawa ulionipa wawe na umoja kama sisi tulivyo na umoja” . Papa alieleza na kumwomba Bwana , asaidie makanisa haya kutembea pamoja, badala ya kulenga katika mgawanyiko . Aliomba uwepo wa upatanifu katika tofauti zinazo watenganisha katika utumishi na hasa kwa wale wanaohitaji zaidi.
Aidha Papa alizungumzia umhimu wa kuwa na ibada za pamoja na matukio mengine ya Wakristo kuabudu pamoja. Alieleza hili huku akiirejea Wiki ya Sala kwa ajili ya Kuombea Umoja wa Wakristo, tukio la kila mwaka mwezi Januari na Siku ya Sala kwa ajili ya Viumbe ya Septemba 1 , kwamba ni matukio mawili ambamo Wakatoliki na Walutheri unaweza kusonga mbele zaidi katika njia hii ya moyo wa kiekumeni.
Mwisho wa maelezo yake Papa alisema “ ni muhimu kwamba Kanisa Katoliki linaendelea kwa ujasiri na kwa uaminifu, kutathmini upya nia za kuwa na Mabadiliko ndani ya Kanisa na kwa namna ya kipekee katika wazo la Martin Luther , aliyedai kwamba Kanisa daima ni lazima kuwa na marekebisho. Alieleza kwa kurejea hati ya pamoja inayoandaliwa kwa wakati huu kwa ajili ya Maadhimisho ya Walutheri ya Mabadiliko katika Kanisa 'Kutoka migogoro hadi Ushirika :Walutheri na Wakatoliki katika Maadhimisho ya Mabadiliko ya Kanisa 2017'. Papa amefurahia juhudi hizo akisema ni njia nzuri yenye matumaini.
Hii ilikuwa ni mara ya tatu kwa Papa Francisco kutembelea na viongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Roma, kama pia ilivyofanyika kwa watangulizi wake, Mstaafu Papa Benedict XVI, Machi 2010 na Papa Yohana Paulo II, Desemba 1983, kuashiria miaka mia 5 ya kuzaliwa Martin Luther.
All the contents on this site are copyrighted ©. |