2015-11-14 07:32:00

Askofu mkuu Gugerotti ni Balozi Ukraine; Askofu mkuu Gualtieri Balozi Comoro!


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Claudio Gugerotti kuwa Balozi wa Vatican nchini Ukraine. Hadi kuteuliwa kwake, Askofu mkuu Gugerotti alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Bielorussia. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Paolo Rocco Gualtieri kuwa mwakilishiwa kitume kwenye Visiwa wa Comoro. Askofu mkuu Gualtieri pia ni Balozi wa Vatican nchini Madagascar, Mauritius na Visiwa vya Ushelisheli.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.