Jumapili wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana, baada ya hotuba yake juu ya Sikukuu ya Watakatifu wote, alionyesha kujali hali ya Mateso ya watu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati na kuziomba pande zote zinazohusika na mduara wa mzozo huu wa kisiasa zijenge moyo wa kuketi pamoja kwa ajili ya majadiliano yanayoweza kutoa jibu la kusitisha ghasia hizo.
Na kwa namna ya kipekee alisema , yuko karibu na Mapadre wa Shirika la Wakomboni walioko katika Parokia ya Mama yetu wa Fatima ya Mjini Bangui , ambao wamepokea mamia ya wakimbizi . Papa alionyesha pia mshikamano wake na Kanisa na jumuiya zote za kidini akiziombea, ili waweze kushinda kila nguvu ya ushindaji wenye kuleta mgawanyiko na utengano katika kuichukua njia mazungumzano kwa ajili ya kufanikisha amani. Na amewahimiza Wakristo na wote wenye mapenzi mema, daima wawe mfano halisi wa huruma ya Mungu na Maridhiano . Papa Francisco ana Mpango kufanya ziara ya Kitume Jamhuri ya Afrika Kati hapo tarehe 29 Novemba 2015.
Aidha wakati huo wa sala ya Malaika wa Bwana , alilikumbuka tukio la Kutajwa kuwa Mwenye Heri, Mama Tereza Casini, Mwanzilishi wa Shirika la Masista wa Oblate wa Moyo Mtakatifu wa Yesu . Sista na Mmisionari aliyethamini sana Ibada na sala za kuabudu na matendo menma. Papa alitoa shukrani kwa ushuhuda wake wa maisha.
Na nyakati za jioni Papa alikwenda katika Makaburi ya Verano yaliko nje kidogo ya Jiji la Roma kwa ajili ya kukamilisha maadhmisho ya Siku kuu ya Watakatifu wote. Mahali hapo, pia hotuba yake ilitafakari mafundisho ya Yesu juu ya Heri aliyoyatoa katika kilima karibu na Ziwa Galilaya. Papa alisema mafundisho ya Yesu, Bwana Mfufuka na hai , yanatuonyesha hata sisi leo hii , njia tunayopaswa kutembea , ambayo iko kinyume na furaha za kidunia. , Yesu alisema, mwenye kutembea katika njia hiyo, huwa na maisha yenye furaha siku zote , ingawa kwanza anaweza ona kama ni mateso lakini hatima yake ni kuwa na furaha kamili.
All the contents on this site are copyrighted ©. |