2015-11-02 09:28:00

Katika Kipindi cha Mwaka 2014- 2015 Kanisa limewapoteza viongozi 115


Baba Mtakatifu Francisko, Jumanne tarehe 3 Novemba 2015 anatarajiwa kuadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya kuwakumbuka na kuwaombea Marehemu Makardinali pamoja na Maaskofu wote waliofariki dunia katika kipindi cha mwaka mwaka 2014 hadi Oktoba 2015. Katika kipindi hiki, Kanisa limepoteza Makardinali 15, Patriaki 1 pamoja na Maaskofu 99 kutoka sehemu mbali mbali za dunia.

Kutoka Barani Afrika, Kanisa limewapoteza Maaskofu 10 kati yao kutoka katika Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki na Kati, AMECEA ni watatu nao ni kama ifuatavyo: Askofu mkuu mstaafu James Spaita wa Jimbo kuu la Kasama, Zambia, Askofu Joseph Mukasa Zuza wa Jimbo Katoliki Mzuzu, Malawi pamoja na Askofu mstaafu Magnus Mwalunyungu wa Jimbo Katoliki Tunduru-Masasi, Tanzania. Wote hawa tunawaombea raha na mwanga wa milele viweze kuwaangazia daima.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.