2015-10-29 15:29:00

Jubilei ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Chama cha Wafuasi wa Kristo!


Baba Mtakatifu Francisko katika maadhimisho ya Jubilei ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Jumuiya ya Wafuasi wa Kristo “ Legionari di Cristo” na Wachama wa Chama cha Ufalme wa Kristo “ Regnum Christi” ametoa rehema kamili kwa wale wote watakaofuata na kutekeleza masharti yanayotolewa na Mama Kanisa ili kuweza kupokea rehema kamili. Maadhimisho haya yatafungwa rasmi kunako mwaka 2016 katika maadhimisho ya Siku kuu ya Moyo Mtakatifu wa Yesu, ambayo pia imetengwa maalum kwa ajili ya kuombea utakatifu wa maisha na utume wa Kipadre.

Hati ya rehema kamili imetiwa sahihi na Kardinali Mauro Piacenza, Mkuu wa toba ya kitume baada ya kupokea maombi yaliyotolewa na Mkurugenzi mkuu wa Chama cha Wafuasi wa Kristo na Chama cha Ufalme wa Kristo padre Eduardo Robles-Gil. Lengo na maombi haya ni kuwawezesha wanachama kujikita katika maisha na utume wao, kwa kuonesha uaminifu katika maisha ya Kikristo, wito wa Kipadre, maisha ya kitawa pamoja na kusimama kidete kulinda na kutetea Injili ya familia kadiri ya Mafundisho tanzu ya Kanisa.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.