2015-10-24 10:43:00

Papa awaombolezea mahujaji 43 waliofariki dunia kwa ajali ya gari!


Baba Mtakatifu Francisko ametuma salam za rambi rambi kwa Askofu mkuu Jean-Pierre Ricard wa Jimbo kuu la Bordeaux kufuatia ajali mbaya ya gari kati ya Bus na Lori kugongana uso kwa uso huko Puisseguin, Bordeaux, Ufaransa Ijumaa tarehe 23 Oktoba 2015 na kusababisha watu 43 kupoteza maisha. Hii ni kati ya ajali mbali kuwahi kutokea nchini Ufaransa katika kipindi cha miaka thelathini iliyopita.

Katika salam zake za rambi rambi zilizotumwa kwa niaba yake na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican, Baba Mtakatifu Francisko anapenda kuungana na wote wanaoomboleza kutokana na msiba huu mzito pamoja na kuwaweka marehemu wote chini ya ulinzi na huruma ya Mwenyezi Mungu, ili aweze kuwapokea na kuwaonesha mwanga wa amani. Baba Mtakatifu anapenda pia kuwafariji majeruhi wote na kuwaombea ili waweze kupona haraka na kuendelea na shughuli zao.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.