2015-10-22 14:24:00

Mchango wa Kardinali Max kwa wanahabari siku ya Jumatano


Kardinali Reinhard Marx, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Ujeruman akizungumza na wanahabari siku ya Jumatano alisema hata kama wanadoa wanatengana, Kanisa bado lina wajibu wa  kutembea pamoja na wanandoa hao waliotengana. 

Aidha aliwaambia wanahabari kwamba, kuandikwa kwa  hati ya mwisho ya maoni ya Mkutano wa Sinodi, haina maana ya kuwa ndiyo hatima ya majadiliano katika masuala yanayohusiana na ndoa na familia. Hati hiyo inayounganisha michango ya maoni zaidi ya 500 yaliyotolewa, inakuwa ni rejea katika mwendelezo wa majadiliano kunapojitokeza matatizo kati ya wanandoa. Kardinali Reinhard Marx, aliendelea kueleza kwamba, mafundisho ya Kanisa ni msingi wa familia ilianzishwa na mume na mke, watu walio sema "ndiyo",mbeleya altare kwamba wanataka  kuwa pamoja "milele", na kuzaa  watoto. Na Kanisa, aliongeza, lazima liwe tayari kukabiliana hata katika uso wa kushindwa kwa ndoa.

Kanisa linawataka wanandoa kuwa aminifu katika ahadi zao." Ni lazima na muhimu kuwa aminifu hata kwa ndoto zetu" alisisitiza na kuongeza ni dhahiri. ni muhimu kuwa na utambuzi kwamba,  Kanisa linazingatia mafundisho yake,  kwa kuwa ni muhimu kwa wanandoa na jamii kwa ujumla, katika kuwa na jumuiya yenye kujiheshimu na iliyo starabika. Kardinali alieleza na kuhoji  kuna nini hasa  nyakati hizi kinachosababisha ndoa nyingi kutodumu? Kanisa lina jibu gani nini? Kanisa lazima aliongeza  kutembea pamoja na hata wale wanao legea au kushindwa kuziishi ahadi zao. Kanisa lazima liwe pamoja na wote wanaolemewa na matatizo  na wale wanaoshindwa kubeba matatizo. Hli ndilo lilikuwa kiini cha majadiliano.

Ni lazima kwa hiyo alisisitiza "kukaa pamoja" na Kanisa, kujaliana mmoja kwa mwingine,licha ya makosa tunayofanya.  Rais wa Baraza Ujerumani Maaskofu, alirejea msisitizo uliotolewa na Baba Mtakatifu juu ya ndoa na familia kwamba ni mtima wa Kanisa na jamii, ikiwa ni pamoja na  madhumuni ya kueneza Injili  na ubinadamu duniani. Na kisha alirudia kusema hapana kwa ubaguzi na madhulumu dhidi ya wanawake. Kuhusu itikadi hizo, alisema ni lazima kuwa na utambuzi kwamba, tofauti za jinsia ziliwekwa na Mungu, kwa lengo la kukamilishana. Na hivyo ni lazima hakikisha kwamba, tofauti za jinsia lengo lake  ni kujenga kitu kilicho kamili.  

Na akijibu maswali ya waandishi wa habari kwamba Kardinali Marx  kuhusu mada ya talaka na kuoa au kuolewa tena , alisema kuwa kundi wanaozungumza kijerumani, wamependekeza  pendekezo kwa kauli moja "kwenda zaidi, kuongozana nao katika njia yao, kama fursa ya kufikia  maridhiano na Kanisa." Katika mwelekeo huu, wito kwa Kanisa ni  "kusafiri nao kirafiki".

Na kardinali Daniel Fernando Sturla Brehouet, Askofu Mkuu wa Montevideo Uruguay, yeye  aliwaambia wanahabari kwamba, Kanisa si klabu ya watu waliokamilika, lakini ni  nyumba ambayo milango yake iko wazi kwa wote, wote wanakaribishwa ndani yake wote walio katika shida.

 Aidha Askofu Mkuu Martin Eamon, alitoa  mwaliko mwingine wa Kanisa  kutembea pamoja na jamaa yao, akisema inahitajika kwa wachungaji na kanisa kuwa na subira siku zote. Wanahitaji daima kujiuliza nini cha kufanya , iwe kwa wiki hii, wiki ijayo miezi ijayo au miaka ijayo , kwa ajili ya kufanikisha maisha kamilifu ya ndoa na familia.  








All the contents on this site are copyrighted ©.