Baba Mtakatifu Francisko, kwa njia ya telegramu iliyotiwa saini na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, amepeleka salaam na ujumbe wake kwa Askofu Nazzareno Marconi, wa Jimbo la Macerata - Tolentino - Recanati - Cingoli - Treia, juu ya tukio la mkutano wa kimataifa wa Matazamio mapya kutoka tafakari Padre Matteo Ricci. Mkutano huu wa Kimataifa wa siku tatu Oktoba 21 hadi 23, umeandaliwa na Chuo Kikuu Macerata na Taasisi ya Confucius Macerata.
Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake ameonyesha furaha yake na kutoa shukrani kwa hatua hii ya kuimarisha kazi ya kimisionari na utamaduni watu Macerata, wapenzi wa rafiki wa watu wa China. Na kwamba utakatifu wake Padre Ricci ,umetengeneza mfumo wa uhusiano kati ya utamaduni wa Ulaya na China, wenye kuthibitisha umuhimu wa mazungumzo kati ya tamaduni na dini katika kuheshimiana kwamba huzaa matunda kwa manufaa ya wote. Kwa hisia hizo, Ujumbe wa Papa, umewatakia wote wanaoshiriki katika mkutano huo, kila mafanikio, na pia amewakumbuka waandaaji, wasemaji na watazamaji wote matashi mema na kuwapa baraka zake.
Katika siku hizi tatu za mkutano unatazama zaidi adhimisho la kupita miaka mitano, tangu 2010 , ya kufanya kumbukumbu ya miaka mia nne tangu kilipotokea kifo cha mmisionari Padre Ricci, o wa Macerata. Mkutano unaendeshwa kwa nia kuwakutanisha wanasayansi kutoka China, Ulaya na Marekani, kujadili kwa kina majitolea na mafunzo ya Ricci , kwa hamu kubwa kutoka kwa Xu Lin, Rais wa Mkoa wa Hanban China na Naibu Waziri wa Elimu, ambaye alizindua wazo la kuwa na mkutano huu wakati alipofanya ziara rasmi katika chuo cha Confucius cha Macerata mwaka 2013.
All the contents on this site are copyrighted ©. |