2015-10-21 14:26:00

Viongozi wa kiserikali na kidini watakiwa kuheshimu utamaduni mbalimbali


Baraza la Makanisa la Dunia, limetoa wito  kwa viongozi wa kiserikali na kidini kutunza heshima kwa utambulisho tofauti wa mil na desturi za kidini na kijamii si tu Mashariki ya Kati lakini duniani  kote kama njia ya kudumisha amani. Na kwamba amani ya muda mrefu kwa  Mashariki ya Kati itawezekana tu kupitia njia uimarishaji wa utamaduni na dini,  ambayo imekuwa sifa ya mkoa huo kwa karne nyingi.  Ni maoni kutoka kwa  Mchungaji Olav Fykse Tveit, Katibu Mkuu wa Baraza la Dunia la Makanisa (WCC), aliyoyatoa katika Mkutano wa Kimataifa , Jumatatu, mjini Athens.

Mkutano huo  ulifadhiliwa na Serikali ya Ugriki  katika lengo la kujenga umoja na mshikamano kwa  jumuiya na vyama vingi vya kidini, kamassehemu ya juhudi za kujenga umoja na mshikamano  wenye kuwezesha uwepo wa jumuiya hizo za imani, wakiwemo Wakristo,  kutoka nchi mbalimbali, zikiwemo  Iraq na Syria, napamoja na  uwepo wa juhudi za kiekumeni kwa ajili ya kuwaunganisha watu.  Haya yameelezwa katika Ripoti ya  mtandao wa  tovuti ya WCC. 

Katibu Mkuu wa WCC anasema, kama  kweli serikali inaundwa kwa ajili  ya kuhudumia watu, basi inawajibu wa kuzingatia ulinzi  kwa watu wote na hasa waathirika wa aina yoyote ya ghasia. Pia ni  muhimu kuhamasisha michango ya jumuiya za kidini,  mila na imani kuwa watetezi wa amani. Kwa maana hii, Fykse Tveit alisema, ni lazima kama wawakilishi wa dini, kutambua umuhimu huu na  kushiriki katika kutoa sauti thabiti  kwa ajili ya kulinda hadhi ya kila binadamu na haki za watu wenye imani na hata wasiokuwa na imani, kama njia ya kukomesha vurugu zote na katika kukataa matumizi ya silaha kama njia ya kutatua migogoro.

 Mtazamo, huu ni uzoefu wa muda mrefu kama sehemu ya WCC , alieleza Katibu Mkuu Tveit, akiomba ushirikiano na mshikamano wa karibu kati ya  viongozi wa  taasisi za Kiislamu na Kiyahudi, hasa kuanzisha na kuwezesha majadiliano kupitia juhudi za pamoja katika masuala muhimu.

Ni muhimu kwa Mashariki kuzingatia umuhimu wa utume wa Wakristo. Kwa maoni yake Fykse Tveit, katika mkoa wenye matatizo mengi , ambayo yanatuwezesha kumwona Kristo Mteswa,  aliyesulubiwa na  kufufuka hata katikati ya mateso mengi, tunatiwa moyo kwamba, ingawa Wakristo wamebaki wachache katika kanda, bado Wakristo wana imani  kama Yesu alivyosema katika Injili, ni "chachu ndogo ambayo inaibua unga nzima. "

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.