2015-10-20 16:41:00

Padre Lombardi -Muhtasari wa vikao vya Sinodi kwa Siku ya Jumanne


Padre Federico Lombardi, amewaambia wanahabari kwamba, Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya Familia, Jumanne hii 20.10 15 katika kipindi cha asubuhi, ilikamilisha kazi za vikundi vidogovidogo, katika sehemu ya tatu na ya  mwisho katika Rasimu ya kufanyia kazi “ Instrumentum Laboris “ juu ya Mada Utume wa Familia leo hii. Na kwamba, majira ya jioni, kitakuwa ni kipindi cha kuwasilisha maoni kutoka  makundi madogomadogo katika lugha 13 kwa Mababa Sinodi, maoni yatakayo tolewa rasmi na kuchapishwa kesho Jumatano.

Katika mkutano huu wa wanahabari wageni rasmi waalikwa kutoka Ukumbi wa Sinodi walikuwa ni Makardinali tatu: Kardinali Lluis Martinez Sistach, Askofu Mkuu wa Barcelona Hispania,  Kardinali ​​ Wilfrid Fox Napier, Askofu Mkuu wa Durban Afrika Kusini , na Kardinali  Alberto Suarez Inda, Askofu Mkuu wa Morelia, Mexico.

Kardinali Martinez Sistach amesema familia si tu matatizo na changamoto , lakini zaidi ya yote, ni fursa nzuri ya kuwa na furaha.Kardinali Martinez ameeleza na  kusisitiza maandalizi mazuri na ya kina kwa watu wanaotaka kufunga ndoa , na kwamba ni maandalizi haya mazuri ni muhimu kwa wote hata kwa wale wanaotaka kufunga ndoa kwa haraka haraka . Maandazi mazuri yakina na thabiti ni kipengere muhimu kinachoweza kupunguza wanadoa kutaka kutaka kutengana au kuvunja ndoa.  Kwa hiyo, Kardinali alirejea juu ya Waraka Binafsi wa Papa Francisco Motu Proprio, iliyozungumzia  mageuzi katika mchakato wa kubatilisha  ndoa, akisema ni mageuzi yanayolenga katika uwepo wa mapatano na na huruma ya Kanisa,  katika mwanga wa ndoa isiyotanguliwa. Ili kwamba wanaondoa walioshindwa kuyaishi maagano yao ya ndoa waweze kuyajenga maisha yao upya kulingana na ahadi waliyoitoa, mbele ya Mungu na Kanisa.

Kardinal amesisitiza zaidi katika Uhakika na maandalizi mazuri ya wanaohusika katika mahakama za kikanisa, ili kuongeza ufanisi katika utaratibu huo, kwa ajili ya  kupata ukweli wa lengo na mchakato, unatafuta kufupisha kipindi cha kawaida kilichowekwa katika utaratibu wa kawaida.

Na Kardinali Suárez Inda, yeye alizama zaidi katika kukilinda kitengo cha  familia kutokana na umuhimu wake wa kuwa  msingi wa jamii. Kwa  upande wake, Kardinali. Suarez Inda, ameonyesha  matumaini kwamba,  taasisi zote zitaweza kutoa utetezi kwa kitengo cha familia. Kardinali alirejea  hatma ya wahamiaji, ambamo mna matatizo mengi kwa familia si tu kwa sababu ya umbali wa kijiografia, lakini pia kwa kipengele cha udhibiti unaofanywa na sera za kiserikali zenye kuzuia wakati mwingine wanafamilia kuungana. Katika hili,  Kardinali aliwashukuru Maaskofu wa Marekani kwa ajili ya kazi kubwa wanao ifanya ya kuzipokea familia za wakimbizi hasa za wakimbizi kutoka  Mexico.

Akijibu hatimaye maswali ya waandishi kuhusu uwezekano wa Papa kutembelea Mexico, Kardinali. Suarez Inda alisema, ni wazi ziara ya Papa Francisco nchini Mexico ni  jambo la linalo pokelewa kwa mikono miwili na Wamexico hata kama tarehe bado kupangwa. Na kwamba bila shaka Papa, atalenga zaidi katika mandhari ya maridhiano na amani. Na bila shaka Papa atatembelea  madhababu ya Mama Yetu wa Guadalupe na pengine anaweza kupata nafasi ya  kutembelea magereza na kukutana na vijana, kwa lengo la kuwapa  matumaini kwa ajili ya  nchi yao.

Na Kardinali Napier, wa  Afrika Kusini yeye alilenga zaidi katika hisia na matumaini ya Sinodi, na nafasi ya Mkutano huu wa Sinodi kwa bara la  Afrika. Na alitoa hisia zake kwamba, Maaskofu toka Afrika wametoa mchango mkubwa na muhimu katika yale yaliyojitokeza katika sinodi hii hasa matumaini ya Sinodi", kwa kufuata mafundisho ya Kanisa na pia yale yanayotolewa na  Papa Francisko. Na kisha aliangalisha kwa walei, hasa juu ya familia yenye furaha, akisisitiza kwamba , familia hizo ndizo zimekuwa zikitoa mwelekeo wa njia inayofaa kufuatwa na  Sinodi. Kwa hiyo muhimu kuzingatia wito na ujumbe wa familia katika Kanisa leo na kuongozana wanandoa kabla na baada ya ndoa, kwa ajili ya kuleta  mabadiliko chanya katika Kanisa na kuleta mageuzi ndani ya familia, kwa mujibu wa misingi yake asilia.

Hatimaye alisema, Kanisa hufanya  kazi zake katika roho ya umoja kwa manufaa ya kanisa zima. Na hivyo katika Mkutano huu wa Sinodi, wameweza kufanya kazi pamoja Makardinali na  Maaskofu na wamegundua upya maana na umuhimu wa roho ya ushirikiano, jinsi inavyoweza  daima kuleta yaliyo mema na bora zaidi katika maisha ya  kanisa.
 








All the contents on this site are copyrighted ©.