Tarehe 16 Oktoba ni Siku ya Chakula Duniani, ambayo huadhimishwa chini ya usimamizi wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa FAO. Mkurugenzi Mkuu wa FAO, Jose Graziano da Silva, akizungumza katika Mkutano wa Kilele wa Mameya juu ya Siku ya Chakula duniani, mkutano uliofanyika mjini Milan Italia kwa siku tatu, amesema , majiiji yana jukumu muhimu katika kufuta njaa na kuboresha lishe duniani. Na alipokea kwa mikono miwili dhamira ya majiji zaidi ya 100 duniani, yaliyopania kuingiza mifumo ya chakula ya chakula katika sera za majiji kwa ajili ya kuleta usawa zaidi na maendeleo endelevu. Da Silva ametoa shukurani zake za dhati kwa Meya Giuliano Pisapia wa Milani na wenzake toka Majiji ya dunia , kwa kusaini Mkataba wa Milan wa Sera ya Chakula.
Pia ametoa shukrani kwa makubaliano majiji , katika kuambatana na kanuni nne, ikiwa ni : kuhakikisha uwepo wa chakula na afya kwa wote; kukuza mfumo endelevu wa chakula; kuelimisha umma juu ya chakula bora, na kupunguza utupaji wa chakula kama taka. Aliendelea kusema watendaji muhimu kwa sera za mafanikio ya maendeleo endelevu yaliyo katika makubaliano ya duniani nzima, ikiwa ni pamoja na kuondoa njaa ifikapo mwaka 2030, ni Mameya , kutokana na ukweli kwamba watu wengi sasa wanaishi vijijini.
Dr Graziano da Silva, aliibaini, lakini ili kufikia malengo haya, Mameya wa Miji
ni lazima waungwe mkono na sekta zote za maendeleo, tena kwa kipindi kirefu, ikiwemo
pia kushughulikia mabadiliko ya tabia nchi na kupunguza uzalishaji hasa wa mazao.Alieleza
hilo huku akionyesha kutambua kwamba, idadi kubwa ya watu wanaoishi tayari katika
miji, inatarajiwa kuongezeka, hasa katika nchi zinazoendelea. Lakini kwa bahati
mbaya si miji yote yenye kuwa na uwezo wa kuhakikisha upatikanaji imara wa chakula
na maji kwa wakazi wote wa miji. Na hii inatokana na suala la uhakika wa chakula na
lishe kupuuzwa katika mipango ya miji na maendeleo endelevu, amesema Graziano da
Silva.
Mkataba wa Sera ya Chakula wa Milan, ambayo umeandaliwa kwa msaada wa kiufundi na
FAO, unatambua umuhimu wa mbinu shirikishi kati ya serikali, sekta binafsi na asasi
za kiraia.
Pia unatambua umuhimu wa kuboresha uhusiano kati ya maeneo ya mijini na maeneo
ya jirani ya vijijini. Katika hali hii, Mkurugenzi Mkuu wa FAO, ametaja ufumbuzi
bunifu kama vile kutoa msaada wa kuhamasisha ongezeko la idadi ya wakulima wadogowadogo
kandokando mwa miji , kama msaada wa kuziba pengo katika upatikanaji wa chakula kutoka
maeneo mengine mbalimbali na pia kwa ajili ya uboreshaji wa mlo na afya njema kwa
familia zinazoishi mjini. .
Mkataba wa Sera ya Chakula ya majiji , umetolewa kama sehemu ya mipango iliyohusiana
na Maonyesho ya Dunia ya Milan Expo 2015, yaliyofanyika Milan, chini ya Mandhari
"Kulisha Sayari, Nishati kwa Maisha". FAO ni kati ya waratibu shiriki wa Umoja wa
Mataifa katika Maonyesho ya Expo 2015. Maonyesho yaliyohudhuriwa na mamilioni ya
wageni, wakipata fursa ya kujifunza zaidi kuhusu masuala yanayohusiana na usalama
wa chakula, lishe, endelevu, kupunguza umaskini, maendeleo na ushirikiano, na kazi
za Umoja wa Mataifa katika kuwa na dunia isiyo na uso wa njaa.
All the contents on this site are copyrighted ©. |