2015-10-14 08:51:00

Ban Ki moon asisitiza umuhimu wa kuzingatia maarifa na hekima za wahenga


Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Maafa Duniani, ambayo ni kila tarehe 12 Oktoba , Katibu Mkuu wa  Umoja wa Mataifa, Bwana Ban Ki moon ametoa wito wa kutambuliwa kwa  juhudi za jamii, kubwa na ndogo, ambao kwa  hekima yao, ushirikiano wao wa  thamani na  maarifa kwa maisha , waliweza kukabiliana na majanga. Ameandika Katibu Mkuu wa Umoja Bwana Ban ki-Moon katika ujumbe kwa maadhimisho ya mwaka huu, akilenga katika kujenga nguvu ya maarifa ya jadi, asili.

Hotuba yake imetoa mfano mzuri,  wa kimbunga Pam kilichotokea katika bahari ya  Pasifiki mwezi Machi, jinsi ambavyo  hapakutokea maafa makubwa kwa watu kutokana na jinsi makazi yao wameyajenga katika mtindo wa kijadi uliozingatia hali halisi za hewa katika eneo hilo na hivyo  tufani au kibunga  vinapotokea , hakuna madhara makubwa kwa  maisha ya watu wengi.  Ban amesema, "maarifa ya jadi na hekima za wazawa ni msingi muhimu, kwa jamii nyingi zinazopendelea  kuishi kwa amani na katika kukabiliana na matukio asili kama machafuko ya hali ya hewa,  ongezeko la joto na kupanda kwa bahari."

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aliendelea kubainisha kwamba, juhudi za Umoja wa Mataifa akisema, mfumo wa kazi kwa ajili ya kupunguza hatari za maafa,, unatambua umhimu wa  ushiriki wa jamii katika  ngazi zote.  Pia imesisitiza jinsi maarifa ya jadi yanavyoweza  kusaidia elimu ya kisayansi katika usimamiaji wa majanga. Kujenga ujasiri na majanga pia ni kipengele muhimu katika Malengo ya Maendeleo Endelevu, ambayo ni   mwongozo wa juhudi za watu duniani katika kukomesha umaskini na kukuza ustawi wa pamoja katika dunia ya afya ifikapo mwaka 2030.

Aidha Jumapili iliyopita, Mkuu wa Kanisa la Ulimwengu, Papa Francisko , aliikumbuka Oktoba 13, Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Maafa, akisema, "Ni lazima  kuwa na utambuzi  kuwa madhara ya majanga,  mara nyingi husababishwa na kiburi cha binadamu katika  hudumia mazingira.  Papa alieleza hilo  wakati wa sala ya Malaika wa Bwana, aliyosali mbele ya mahujaji na wageni waliokuwa wamekusanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. Papa alisema ni muhimu kwa kila mmoja wetu  kujiunga katika juhudi za kimataifa na serikali za mitaa kwa ajili ya  kupunguza maafa,  kuwa na ujasiri mkubwa katika kupambana  na maafa kwa njia ya kuhuisha elimu mpya na ile ya  jadi kwa makini hasa kwa watu walio hatarini zaidi.








All the contents on this site are copyrighted ©.