Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa FAO, katika taarifa yake ya 2015 juu ya hali ya chakula na kilimo, iliyotolewa kama angalisho kwa Adhimisho la Siku ya Chakula Duniani ambayo huadhimishwa tarehe 16 Oktoba, inasema , licha ya kupanua hifadhi za kijamii na ufuatiliaji kwa kasi, juhudi za kukomesha njaa vijijini,bado zinahitajika kuikomboa idadi kubwa ya watu maskini vijijini, wanaohangaika na uhaba wa chakula na njaa.
Ripoti hiyo ya FAO, inabaini kwamba , leo hii katika nchi maskini , mifumo ya ulinzi wa kijamii, kama vile uhamisho wa fedha, chakula mashuleni na kazi za umma, hutoa njia za kiuchumi kwa watu hawa maskini wanaoishi katika mazingira magumu, ni fursa ya kuondokana na umaskini na njaa ,na hivyo kuboresha afya, elimu na nafasi nzuri kwa maisha ya watoto wao.
Mipango kama hiyo kwa njia mbalimbali inaweza kuwa ya manufaa kwa watu bilioni
2.1 wa nchi zinazoendelea, ikiwa ni pamoja na kuwaweka watu milioni 150 kutoka katika
umaskini uliokithiri.
Kupanua mipango hiyo katika maeneo ya vijijini na kuwaunganisha watu katika umoja
wa sera ukuaji wa kilimo, kunaweza leta kasi katika kupunguza idadi ya watu maskini,
inasema ripoti hiyo.
Ripoti hii imetolewa kama utangulizi kwa ajili ya Siku ya Kimataifa ya Chakula (16 Oktoba), ambayo hulenga kutazamisha watu kwa makini juu ya hali ya hifadhi za kijamii, kama hatua ya kuvunja mzunguko wa umaskini vijijini.Mkurugenzi Mkuu wa FAO, Josè Graziano daSilva anasema , hii ni hoja ya kidharura inayotaka kuungwa mkono , katika kusaidia watu wanaoishi katika mazingira magumu, kuondokana na adha ya njaa duniani ..
All the contents on this site are copyrighted ©. |