2015-10-08 16:31:00

Taratibu mpya za ndoa kuanza kutumika Desemba


Marekebisho katika taratibu za mchakato ndoa zinazotafuta kubatilishwa, yaliyotolewa  katika barua binafsi ya Papa  Francisco Motu Proprio iliyotolewa Septemba 8,2015,  na uhusiano wake na Sinodi mbili za ndoa na familia, kwa ajili ya uboreshaji wa utendaji wa kanisa katika kufanikisha kwa wepesi na urahisishaji wa utendaji wa Maaskofu wote duniani, katika umuhimu wa kutoa maamuzi ya Askofu, na tathimini mpya katika sheria ya ndoa katika Jimbo Kuu , ni kati ya mandhari zinazo shughulikiwa na Mahakama  Rota Romana.   Ni maelezo yaliyotolewa na Dekano Pius Vito Pinto wa Mahakama ya Rota Romano, kwa gazeti la L’Osservatore Romano. Maelezo yake ameyatoa ikiwa umepita mwezi mmoja baada ya kupitishwa ya hati mbili za kisheria za Papa ,  zitakazoanza kufanya kazi Desemba 8 mwaka huu , ambao ni mwanzo wa Jubilee ya Mwaka wa huruma ya Mungu .

Mons. Pinto amezungumzia juu ya mageuzi makubwa yaliyofanyika , ambayo tayari katika siku hizi za mwanzo wa Sinodi , yalipokewa vyema kama  sheria iliyo wazi,  katika kukabiliana na mahitaji ya haraka ya waamini na kama ambavyo Papa anatarajia kuwajengea waamini matumaini, na si kuwaweka katika hofu.

Aidha ametoa maelezo juu ya  uhusiano kati ya mbili nyaraka Papa na Sinodi akisema, Motu propri mbili zilizotolewa na Papa ni  matokeo ya kutembea pamoja Kisinodi, na nyenye kuonyesha umoja wa halisi ya Maaskofu. Na kama inavyofahamu, kabla ya nyaraka hizi mbili kutolewa kulikuwa na mashauriano mapana juu ya suala hili.  Kwa hiyo Papa ametoa nyaraka zake kutokana na uzoefu mkubwa Maaskofu, ulioonekana katika kujibu maswali yaliyotumwa katika Mabaraza yote ya Maaskofu yote.  Ni matokeo ya majibu ya muungano mpana wa Maaskofu katika haja ya kuboresha na kurahisisha taratibu za kesi za ndoa kama ilivyo sisitizwa katika Kipengere namba  115 cha hati ya kufanyia kazi “Instrumentum Laboris”, na kama alivyo eleza Kardinali Erdo Baldisseri na katika ripoti yake ya  ufunguzi wa mkutano wa XIV wa Sinodi.

Ni kuhuisha na kurahisisha taratibu: katika maana yake ya kina na halisi, kama ambavyo tayari ilikwisha tamkwa na Papa Pio X , mwanzoni mwa karne ya ishirini,akilenga kurudisha kikamilifu taratibu za uwezo wa  mahakama katika majimbo na majimbo makuu.   Kwa njia hii, Papa Francisco  anataka kurudisha ukaribu zaidi wa  miundo ya utendaji wa Kanisa kwa waamini.








All the contents on this site are copyrighted ©.