Jumatatu 04 Oktoba 2015, majira ya asubuhi, katika ukumbi wa Mikutano ya Sinodi wa Vatican, kulianza vikao vya Sinodi ya XIV ya kawaida ya Maaskofu, ikiongozwa na Kauli mbiu: Wito na Utume wa Familia:Ndani ya Kanisa na Ulimwengu mamboleo. Sinodi hii iliyokutanisha Maaskofu na wajumbe wateuliwa kutoka pande mbalimbali za dunia itaendelea kwa muda wa wiki tatu hadi tarehe 25 Oktoba 2015.
Katika siku yake ya kwanza, ratiba inaonyesha kwamba, Baba Mtakatifu Francisco, anashiriki vikao vya Sinodi mara mbili , asubuhi majira ya saa tatu na pia jioni majira ya saa kumi za jioni.
Katika kikao cha asubuhi, alitoa mchango wake wa kwanza cha Mkutano huu, akisema
kwa hakika, jambo hili lilianza muda mrefu kabla,kwa ajili ya kutathmini na kutafakari
yaliyomo katika rasimu ya kufanyia kazi( Instrumentum Laboris) mada hii: Wito na
Utume wa Familia ;Ndani ya Kanisa na Ulimwengu mambo leo ,na utoaji wa fafanuzi juu
ya jukumu la sinodi na majibu kutoka Mabaraza ya Maaskofu na vyombo muhimu husika.
Papa aliendelea kuwakumbusha wajumbe kwamba , sinodi maana yake ni kutembea pamoja,
kwa nia moja na mshikamano, katika ujasiri wa kupitisha yanayotakiwa katika juhudi
za kichungaji na hekima za mafundisho ya kanisa kwa unyofu wa moyo , na daima wakitanguliza
mbele yao, yaliyo mazuri kwa manufaa ya kanisa zima, linaloundwa na familia na mwanga
unaoongoza Roho za watu.
Kwa mara nyingine Papa aliwakumbusha wajumbe kwamba , Sinodi si mkutano, au kama bunge, au kikao cha Maseneta ambavyo hutafuta kufikia makubaliano. Sinodi,ameitaja kuwa ni jina la Kanisa, linalo maanisha kutembea pamoja katika kuusoma ukweli kwa macho ya imani na kwa moyo wa Kimungu; ni Kanisa linaloingilia kati kwa uaminifu yale yanayotatiza kwa amana ya imani, na hivyo mikutano yake si kama mahali pa makumbusho ya kutazama ya kale na wala si mahali tu pa kufanya utetezi, lakini ni chanzo hai ambamo Kanisa hujinywesha yanayoweza kutuliza kiu ya maisha na kumulikia katika hifadhi za maisha.
Kwa hiyo Papa anasema, Sinodi ni hatua ya lazima ndani ya Kanisa na katika taifa takatifu la Mungu, ambamo kama wajumbe wa Sinodi, wanatenda kama sehemu ya kazi za ngazi ya juu za wachungaji, au watumishi wa Kanisa. Sinodi pia ni nafasi ya ulinzi wa Kanisa katika kazi za utendaji wa Roho Mtakatifu. Sinodi huongea kupitia maongozi ya Roho kwa lugha za watu wote wanaoongozwa na Mungu .
Papa alieleza na kuwataka wajumbe wa Sinodi washiriki katika vikao hivi kwa ujasiri wa Roho Mtakatifu, ujasiri wa kitume wenye unyenyekevu na maombi ya Kiinjili bila ya kukatishwa tamaa majaribu ya dunia, yenye kuzima mwanga wa ukweli katika mioyo ya watu. Kuwa na ujasiri wa kitume wenye kuleta maisha mapya na kuyafanya maisha kuwa makumbusho ya kumbukumbu za Kikristo, kwa unyenyekevu wa Kiinjili.
Papa alieleza na kuwasihi wajumbe pia wasikilize kwa ujasiri na makini, hisia za ndani ya moyo wakati wanapo jifunua kwa Mungu, katika ukimya wa sala na hisia zao zote , kuisikiliza sauti ya upole wa Mungu, inayoongea kimya kimya ndani mwao. Papa ameonya , bila kusikiliza sauti ya Mungu, maneno yao yote yatakuwa ni porojo tupu zisizo kuwa na maana . Bila kuongozwa na Roho, maamuzi yao yote ni mapenzi ya kidunia ambayo yatalenga, badala ya kuinua Injili, yataifunika na kuificha.
Na mwisho, alitoa shukurani zake kwa Kardinali Lorenzo Baldisseri, Katibu Mkuu wa Sinodi na wote anaosaidiana nao, Marais wajumbe, waandishi, washauri, watafsiri na wale wote ambao wanashiriki katika kazi za mkutano huu kwa uaminifu kweli na kujitolea kwa Kanisa. Na kwamba wanaianza safari kwa kuomba msaada wa Roho Mtakatifu na maombezi ya Familia Takatifu ya Yesu, Mariamu na Yusufu. Asante sana Papa alimalizia.
All the contents on this site are copyrighted ©. |