2015-10-05 15:41:00

Hotuba ya Kardinali Baldisseri, yazindua michango ya Mababa wa Sinodi


Kardinali Lorenzo Baldisseri, Katibu Mkuu wa Mkutano wa XIV wa kawaida wa Sinodi ya Maaskofu, inayoongozwa na kauli mbiu “Wito na Utume wa familia ndani ya kanisa na Ulimwengu Mambo leo, mapema Jumatatu ikiwa ni siku ya kwanza ya mkutano huu  , alikuwa mtu wa kwanza kutoa mchango wake. Sinodi hii ilifunguliwa Jumapili 04 Oktoba 2015, kwa Ibada ya Misa iliyoongozwa na  Baba Mtakatifu Francisco, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Ibada iliyohudhuriwa na maelfu ya watu.

Kardinali Baldisseri kwa niaba ya Mababa wa Sinodi, alitoa shukurani zake kwa Papa Francisco kwa dhamana aliyowapa, kushiriki katika mchakato huu juu ya wito na utume wa familia, Mada muhimu na nyeti si tu kwa Wakatoliki lakini kwa Wakristo wote na pia ubinadamu wote, na umakini wake katika dhamira za kichungaji za Kanisa. Alieleza na kusema , kama ilivyotangazwa katika Katiba ya Kichungaji juu ya Kanisa na Ulimwengu “Gaudium et Spes katika nyaraka za Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican, ambamo kwa mwaka huu imeadhimishwa miaka 50 tangu uwepo wake, inakuwa  furaha na matumaini , huzuni na uchungu wa watu wa wakati wetu, hasa maskini na wale wanaoteseka, wao ni furaha na matumaini, huzuni na wasiwasi wa wafuasi wa Kristo pia,  hakuna ubinadamu wa dhati unaoweza kuwasahau watu hao katika mtima wa dhati wa moyo. 

Kardinali alieleza na kurejea homilia ya Papa Francisco wakati wa Mkesha wa sala ya kufungua sinodi hii siku ya Jumamosi iliyopita , ambamo Papa alitoa mwangwi wa maneno yaliyorejea katika  kauli mbiu ya kutafakari zao kwamba "Ni muhimu  kusisitiza hata katika  utamaduni binafsi kwamba,  kila binadamu aliyezaliwa na mwanamke,napaswa kuutunza uhai kama jambo muhimu katika  hoja ya kujenga utulivu  mlango wa  uwazi kwenye umuhimu wa mtu kushiriki katika mwendelezo wa maisha na mambo yake mwenyewe.  Papa alieleza ushirika wa maisha huanza tangu wakati wa ndoa , wakati wanandoa wanapojifunua wazi kama zawadi ya maisha na ulinzi wa pande zote. Na kwamba kukutana, uzazi na yatokanayo, mfano  maambukizo ya imani ya Kikristo kwa watoto, wanandoa kama familia huendelea kuwa shule ya ubinadamu isiyokuwa na mbadala, na kituo cha lazima katika kutoa  mchango wa haki na udugu jamii.

Aidha Kardinali Baldisseri ataja utaratibu utakaofutwa katika kupata habari kutoka ukumbi wa Mkutano wa Sinodi akiweka bayana kwamba, Chanzo Msingi cha habari zote zinazotolewa katika vikao vya Sinodi itakuwa Mkurugenzi wa Ofisi ya habari ya Vatican. Na kwa Mababa wa Sinodi wataweza kutoa maelezo yao mmoja mmoja kwa Tume ya Habari. Aidha kwa mwaka huu pia habari muhimu  zitakuwa zikitolewa  kwa ufupi, kupitia ukurasa wa Tweet. Na Mababa wa Sinodi watakuwa huru kufanya mawasiliano na vyombo vya habari kwa hiari  na uwajibikaji wa kutunza siri za majadiliano ya vikao na pia majadiliano ya makundi madogomadogo.

Na kama ilivyokuwa mwaka jana, wametimiza hamu ya kazi za vikao vya Sinodi,  visindikizwe daima na sala kutoka Kania Kuu la Mtakatifu Bikira  Maria  Mkuu la hapa Roma , ambako kwa ushirikiano na Jimbo la Roma, Waamini wataendelea kusali kila siku kwa ajili ya Sinodi katika Kanisa dogo la Bikira  Maria wa “SalusPopuli Romani. Mahali hapo pia kutaweka masalia ya Mtakatifu Tereza wa Mtoto Yesu na wazazi wake Wenye Heri Zelie na Louis Martin, ambao watatangazwa  Watakatifu na Papa Francisco Jumapili ya tarehe 18 Oktoba sanjari na Siku ya Misioni Duniani .

Mapema asubuhi Mababa wa Sinodi walianza kikao cha kwanza cha Mkutano wa Sinodi na Wimbo wa Njoo Roho Mtakatifu Muumbaji, na pia waliomba msaada wa Mama Bikira Maria ,Mama wa Kanisa na Malkia wa Familia, wakikumbuka pia maneno ya Baba Mtakatifu aliyoyatoa akiwa katika ziara ya kitume Cuba hivi karibuni kwamba, “familia si tatizo , lakini zaidi ya yote ni upendeleo. Upendeleo tunaotakiwa kuuhudumia kuutetea na kuandamana nao. 








All the contents on this site are copyrighted ©.