Baba Mtakatifu Francisco kabla ya kusali sala ya Malaika wa Bwana , Jumapili hii , hotuba yake fupi iliwakumbuka watoto wengi walio katika mateso ya kuvikimbia vita katika maeneo yao ambao kwa sasa wanapiga hodi katika milango yetu wakiomba msaada na kupokewa. Aidha alipeleka mawazo ya waliokuwa wakimsikiliza kwa Sinodi ya Maaskofu ya XIV, kuhakikisha "dhamira ya kutosha kwa ajili ya familia na jamii. Aidha aliomba sala za waamini ili dunia iweze kuwekwa huru dhidi ya vita, na pia aliwakumbuka kafara wa maporomoko ya aridhi huko Guatemala na Ufaransa .
Papa alieleza hayo, muda mfupi kupita baada ya kuongoza Ibada ya Misa kwa ajili
ya kufungua Mkutano wa Sinodi ya Kawaida ya Maaskofu wa XIV, iliyoanza leo 4 Octoba
na kuendelea hadi 25 Oktoba 2015. Alitaja nia ya Sinodi hiyo akisema kuwa ,
Mababa wa Sinodi, waliotoka kila sehemu ya dunia na kukusanyika karibu mwandamizi
wa Petro, kwa muda wa wiki tatu, watatafakari juu ya “Wito na utume wa familia, katika
Kanisa na katika jamii, kwa utambuzi makini wa kiroho na Kichungaji”.
Papa amesema, katika wiki hizi tatu, wanayakaza macho yao kwa Yesu, ili kupata,
misingi ya mafundisho ya Yesu ya kweli na huruma yake katika njia sahihi zaidi,
kwa dhamira ya kutosha ya Kanisa na familia na kwa ajili ya familia zote, ili kwamba
mpango asili wa Muumbaji kwa mwanamume na mwanamke uweze tekelezwa kupitia kazi yake
nzuri na nguvu yake katika dunia ya leo.
Papa alieleza kwa kurejea liturujia ya Neno ya Jumapili hii , ambayo maandishi yake
yana msingi wa mwanzo katika kusaidiana na usawa kati ya mwanamke na mwanaume (Mwa
2.18-24). Papa alieleza na kunukuu maneno ya Biblia yanayosema kwa ajili hii mwanamume
atamwacha baba yake na mama yake, ataungana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili
mmoja. Alifafanua kuwa ni maisha ya watu wawili ambayo kwa sakramenti ya ndoa yanaungana
na kuwa kitu kimoja na sawa. Na hivyo wanandoa katika usawa huo wanapokea jukumu
la kuendeleza maisha ya binadamu mpya kama wazazi. Kushiriki katika ubunifu na nguvu
za uumbaji za Mungu mwenyewe. Lakini pia wanatakiwa kuwa makini! Mungu ambaye ni upendo,
anaichukua sehemu ya kazi yake nyeti yake ya uumbaji, na kuidhaminisha kwa viumbe
katika hali ya upendo pamoja naye na kama Yeye .
Kwa maana hii -. Kama Mtakatifu Paulo anavyosema - upendo amekwisha miminwa mioyoni
mwetu kwa njia ya Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi (Rum 5 , 5). Na hii pia ni upendo
ambao unatolewa kwa wanandoa katika sakramenti ya ndoa. Papa alieleza na kusema, ni
upendo ule ule, katika Injili ya leo, Yesu anaonyesha kwa watoto: "Waacheni hao watoto
waje kwangu, wala msiwazuie, kwa maana wao ni warithi wa kweli wa Mungu wao" (Marko
10:14).
Papa aliendelea kueleza kwamba, wakati huo walikuwa wakitolea maombi kwa Bwana, ili
kwamba, wazazi wote na walimu kama pia ilivyo jamii yote duniani, awafanye wote kuwa
chombo cha kuwapokea kwa upendo ulio unadhihirisha na Yesu kwa watoto wadogo. Yeye
huonekana ndani ya nyoyo zenye huruma na wasiwasi kwa baba na mama, wanaopata kwa
wakati mmoja juu ya watoto wao . Papa kwa mawazo hayo , alionyesha kuguswa na mahangaiko
na mateso ya watoto wengi wenye njaa au waliotelekezwa , wanaodhulumika , au kulazimishwa
kufanya kazi za kijeshi kama wapiganaji au wapagazi, na hata wale wanakataliwa na
familia zao kutokana na hali zao za udhaifu wa mwili n.k . Alisema hujawa na simanzi
na uchungu mkali, pale anapotazama picha za watoto waliojaa uchungu , ambao wako katika
harakati za kukimbia umaskini na migogoro, wenye kugonga kwenye milango yetu na mioyo
yetu, wakiomba msaada. Papa alimwomba Bwana, atusaidie sisi kutokuwa ngome ya nguvu
ya ukatili wa jamii, bali tuwe familia na jamii yenye uwezo wa kuwapokea wote kwa
mujibu wa sheria sahihi.
Papa alikamilisha hotuba yake kwa kuomba sala za waamini zisindikize kazi za Sinodi, ili kwamba Roho Mtakatifu afanye kazi yake ndani ya mioyo ya Mababa wa Sinodi kikamilifu na kwa utulivu na maongozi yake. Na aliomba maombezi Mzazi wa Yesu, Bikira Maria, kuungana na wote kiroho, ambao, kwa wakati huu, wamekusanyika katika Madhabahu ya Mama yetu wa Pompeii, kuomba neema na baraka kwa Mama yetu wa Rozari.
Baada ya sala ya Malaika wa Bwana, Papa alikumbuka tukio la kutajwa kuwa Wenye Heri huko Santander, Hispania, Mtumishi wa Mungu Padre Pio Heredia na wenzake kumi na saba wanashirika wa Cistercian wa Mtakatifu Bernardo, waliouawa kwa kukataa kuikana imani yao wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Hispania na mateso ya kidini katika wakati wao. Papa alisema “Tunamsifu Bwana kwa ujasiri wa mashahidi hawa, na hivyo tunaomba maombezi yao, na kuyaweka kwa unyenyekevu majanga yote ya vita yanayotokea hata kwa nyakati hizi”. Na aliwashukuru wote waliotoka maeneo mbalimbali kwa ajili ya kushiriki katika Ibada hii. Na kwa ajili ya Siku ya Mtakatifu Francis wa Assisi, Mtakatifu mlinzi wa Italia. Kwao wote aliwapa salaam zake za upendo, na kuwaomba wasimsahau katika sala zao.
All the contents on this site are copyrighted ©. |