2015-10-04 15:49:00

Papa : Mkesha wa sala ya kuombea Sinodi ya Maaskofu ya XIV juu ya Familia


Baba Mtakatifu Francisco Jumamosi 03 Oktoba 2015, aliongoza Ibada ya  Mkesha wa sala kwa ajili ya ufunguzi wa Sinodi ya Maaskofu ya kawaida ya XIV.

Papa alianza homilia  yake kwa kuhoji , kuna faida gani kuwasha mshumaa ,mdogo katika giza linalowazunguka? Na je hapakuwa na kitu kingine kilichokuwa na uwezo wa kuondoa giza hilo ? Na je inawezekana kuuzuia mwanga kulishinda  giza?

Papa alieleza na kusema katika vipindi fulani vya maisha , wakati maisha yanapokabiliwa na hoja za nguvu na maswala yanayo shinikiza kwa nguvu kupata ahueni za harakaharaka katika madai ya maisha, mtu huvutwa na kishawishi cha kurudi nyuma  katika jangwa la kiroho na kujifungia ndani, kwa kudhani kwamba ni busara kujiepusha kwa namna hiyo  wajibu wa kutekeleza yale yanayotakiwa kufanyika katika utumilifu wake. 

Papa Francisco alieleza, kwa kukumbusha uzoefu wa maisha ya Nabii Elia,  wasiwasi wa kibinadamu, unaibua  hofu kama ilivyokuwa kwa Nabii huyo , kutoka na kwenda kutafuta makazi mapya alipodhani anajisalimisha . Elia kwa  hofu, aliondoka na kwenda zake kujiokoa [...] akaendelea katika siku arobaini mchana na usiku mpaka mlima wa Mungu, hata Horebu. Papa alieleza yaliyomkabili Elia ,mbele ya uso wa Mungu , kama ilivyoandikwa katika kitabu cha  (1 Wafalme 19,3.8-9).

Papa alisema kwa mtazamo huo , pia mwaka mmoja uliopita , katika uwanja huo wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro,walimwomba Roho Mtakatifu , aiweke Mada ya familia kwa Mababa wa Sinodi, kupata utambuzi na kusikiliza kwa makini wakiwa wamekaza nyuso zao kwa Yesu , mwenye kuw ana neno la Mwisho la Baba na ufafanuzi wa vipengere vyote.

Na katika jioni hiyo, alisihi maombi yao yasiwe kwa mengine , kwa sababu kama  AskofuMkuu Ignatius IV Hazim, alivyokumbuka daima  kwamba bila Roho Mtakatifu, Mungu anakuwa mbali, Kristo anabaki kuwa aliyepitwa na wakati, na Kanisa hubaki kuwa mkusanyiko wa watu usiokuwa na maana, kuwa  mamlaka ya kiutawala wa kidunia na ujumbe  wake kuwa propaganda za utamaduni, wenye utendaji wa kuwaingiza  Wakristo katika utumwa maadili kama ilivyolezwa kaitka mkutano wa Kiekumeni wa  Uppsala, 1968.

Papa aliwasihi wote waliokuwa wakimsikiliza, wasali ili kwamba, kwa Sinodi inayofunguliwa kesho, iweze kuleta picha kamili ya uzoefu wa mtu katika maisha ya ndoa na familia; kutambua, kutathimini na kupendekeza yapi yaliyo mazuri zaidi , katika kuyafanya maisha ya ndoa na familia kuwa mazuri zaidi na matakatifu, licha ya kukabiliwa na mazingira magumu, mtihani wa umaskini, vita, magonjwa, misiba, mahusiano yenye majeraha na matatizo mengi nyenye kuisonga roho  kama chuki na kushindwa. Papa aliomba kuzikumbuka familia na  jamii yote inayokabiliwa na matatizo, kwa mwanga wa Injili, ili kwamba "habari njema" daima iwepo kuapoa na hayo yote. Papa aliendelea kuomba kutoka  hazina ya maisha na mapokeo ya utamaduni, Mababa wa Sinodi, waweze kutoa neno la faraja na matumaini kwa familia zote zilizoitwa katika wito huu wa kujenga mustakabali wa jumuiya ya kanisa na mji wa mwanadamu.

Papa ameomba kila familia, katika ukweli wake iwe  daima mwanga wa maisha Matakatifu hata katika  giza la dunia. Na ndivyo kwa Yesu Mshindi wa giza la Dunia , aliishi ndani ya familia na miongoni mwa jamii, ndani ya familia kama wengine wote wake kwa waume kwa miaka thelathini ya maisha yake hapa duniani, akiwa mbali na ukuu wake wa kifalme.

Papa alieleza na kutolea mifano ya maisha ya watu wengine kama Charles de Foucauld, akiomba familia iwe  sehemu ya maisha matakatifu ya Kiinjili , na katika njia yake ya maisha ya kawaida kwa vizazi na vizazi. Familia kuwa mahali pa utambuzi, ambapo watu wanajifunza kutambua mpango wa Mungu katika maisha yao na kukubaliana na hilo kwa uaminifu. Patambuliwe kuwa makao makuu ya faraja,  busara, udugu na urafiki, mahali panapofundisha moyo wa kukubali wengine na kuwa na moyo wa kusamehe.

Papa alieleza na kuirejea familia Takatifu ya Nazareti iwe mfano katika majadiliano yote ya Sinodi hii inayozungumzia familia.  Na watu wapate utambuzi wa kina kwamba , Kanisa ni mama, na lina uwezo wa kuzalisha maisha na daima hutoa maisha yake kwa ajili ya kuongoza kwa huruma na nguvu ya kimaadili. Papa ameonya kama Kanisa haliwezi kuongoza kwa huruma na kwa haki, basi linapoteza  uhalali na nguvu yake na kuwa halina faida bali lililojaa madhulumu.

Papa analitaja Kanisa kuwa ni nyumba iliyo wazi , iliyo mbali na vigezo vya nje, lenye kuwapokea waamini wake wote bila kujali hadhi ya mtu lakini kwa kila anayesadiki kwa  matumaini ya amani  ya aliye ndani ya kila mtu, ikiwa ni pamoja na wale  waliokata tamaa katika maisha na wale walioumizwa  moyo na mateso.
Kanisa hili linatakiwa kuwa tayari hata kujiweka hatarini kwa ajili ya kumwangazia mtu nuru katika giza la maisha ya mtu, kwa uaminifu kwa lengo na kushiriki katika hatua za maisha , kwa sababu Yeye  Yesu Kristo Mkombozi wa dunia, kwanza aliishi maisha haya ya kidunia kwa ajili ya kufanywa upya kwa moyo wa huruma wa Baba








All the contents on this site are copyrighted ©.