2015-10-04 14:17:00

Homilia ya Papa katika ufunguzi wa Sinodi ya Kawaida ya Maaskofu


Jumapili  Oktoba 4 , 2015 Papa Francis alifungua Sinodi ya Familia kwa Ibada ya misa takatifu katika Basilika ya Mtakatifu Petro.Katika Homelia yake alisema:Tukipendana , Mungu hukaa ndani yetu na pendo lake limekamilika ndani yatu. Baba mtakatifu ameanza akisema maneno ya Mungu katika Domenica hiyo utafikiri ilichaguliwa kwa lengo la ufunguzi wa Sinodi  ya Maaskofu aliyoifungua yeye rasmi.

Baba Mtakatifu alielezea juu ya upweke wa Adamu kwenye Bustani ya Eden, baada ya kupewa madaraka ya viumbe wengine, lakini bado alijisikia upekwe” nimtafutie wa kumsaidia anayefanana naye.(Mw 2,20) Baba mtakatifu aliorodhesha baadhi ya mambo yanayoletwa na upweke akisema kwamba, Katika dunia ya leo bado upweke ni tatizo kubwa linalowasumbua wanaume na wanawake, ukifikiria wazee wanao achwa na watoto wao , wajane wote, na watu wengine wanaume na wanawake wanaotengana katika ndoa zao, ni watu wengi wanaojisikia upweke, hawatambuliwi na wala kusikilizwa, kama vile, wahamiaji  na wakimbizi waliokimbia vita na mateso, vijana wengi waathirika wa utamuduni wa kutumia hovyo, na kutupa hovyo, na pia utamaduni  wa ubaguzi.

Leo watu wanaishi katika utandawazi , wengi wanaonekana  wanaishi katika nyumba za kifahali na kwenye magorofa marefu  lakini ndani ya nyumba zao hakuna joto la familia.Wanayo mipango mingi lakini hawana muda wa kuonja kile walichopata ,bado kuna haina nyingi za mambo ya anasa, lakini daima ndani ya roho zao ni utupu, mambo ya kijifurahisha ni mengi lakini ueondo ni mdogo , huru ni mwingi, lakini kujitegemea ni kidogo, bado kuna ongezeko kubwa la watu wanaojisikia upweke, lakini hata hivyo bado kuna hata wale wanaozidi kuwa wabinafsi na ufitina, wakifanya vurugu ya kujiaharibu, na pia kuwa watumwa na wa anasa , na pia wa Mungu fedha.Leo hii bado tunaishi kwa namna flani kama vile uzoefu wa Adamu, ambapo upweke una nguvu  sana , familia ikiwa ni picha , kwasababu bado hakuna uvumilivu wa kuendeleza upendo imara na kizazi cha upendo, kama walivyokuwa wametoa ahadi “katika afya  na magonjwa, katka utajiri  na katika umasikini, katika wema na ubaya.”

Upendo wa kudumu, mwaminifu , wenye uangalifu na imara na wenye rutuba, unazidi kudhiakiwa na kuonekana umepitwa na wakati,kwani inaonekana kwamba jamii zaidi ya kisasa ndiyo iliyo na asilimia kubwa ya kuwa na watoto wachache, na asilimia kubwa ya utoaji wa mimba , ya  talaka , kujiua na uchafuzi wa mazingira na kijamii.Pia zinaonyesha kuwa Mungu ameumba binadamu kuishi katika huzuni au kuwa peke yake, lakini kwa furaha, kwa kushiriki safari yake na mtu mwingine kwamba ni nyongeza; uzoefu uzoefu wa ajabu wa upendo: yaani, kwa kupenda na kupendwa; na kuona upendo wake uzazi katika watoto, kama zaburi anasema leo (sawa na Zaburi 128).

UPENDO KATI YA MWANAUME NA MWANAMKE: Maneno hayo yanaonyesha kwamba ni  jinsi gani moyo wa mtu unapata furaha  kama wa yule mtu anayemfanana na kwenda sambamba nayempenda na pia kumtoa katika upweke. Vilvile inaonyesha ya kamaba Mungu hakuumba  binadamu aishi kwa huzuni  au aishi peke yak , bali kwaajili ya furaha , kushirikiana njia ya maisha  na mtu mwengine amabayo ni nyongeza, wali waishi uzoefu wa upendo wa ajabu  yaani kupenda na kupenswa:  na kuona upendo wake katka matunda ya watoto, ilivyokuwa katika  zaburi (Zab 128)

Na hiyo ndiyo ndoto za Mungu kwa kiumbe wake , kuona ya kwamba  unakamilika muungano wa uependo kati ya mume na mke, yaani furaha katika njia ya kawaida , na kutoa uzazi kwa pande zote mbili: na hayo ni sawasa na mfano wa muhtasari wa injili ya Yesu iliyosomwa kwa maneno haya,"Tangu mwanzo wa uumbaji (Mungu) aliwaumba mume na mke: kwasababu hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake, na kuambatana mume na mke nao watakuwa mwili mmoja Kwa hiyo, wao si wawili tena bali mwili mmoja " (Marko 10.6-8; Mwa 1:27; 2:24).

Papa aliendelea kusema : mbele ya swali aliloulizwa la kikejeli , pengine lilikuwa mtego kufanya aonekane hasiyefaha katika  umati uliokuwa ukimfuata, na ya kwamba hao walikuwa wanafanya talaka  kana kwamba haifahamiki vizuri katika torati, Lakini Yesu aliwajibu ukweli ambao  hawakutegemea; akiwarudisha juu ya asili ya uumbaji , ili kutufundisha  ya kwamba Mungu anabariki upendo wa kibinadamu, kwani ni yeye anayeunganisha mioyo ya mume na mke wanaopendana na kuwaunganisha katika umoja usiogawanyika. Kwa maana hiyo lengo la maisha ya ndoa siyo tu kuishi pamoja milele, bali ni kupendana  milele! Na hivyo basi Yesu anathibitisha  utaratibu wa awali na mahali unapotokea.

FAMILIA: Binadamu basi asitenganishe alichokiuganisha Mungu, (Marko 10.9). Papa aliwashauri waumini wote kuondokana na aina za ubinafsi , na pia sheria ambazo zinaficha ubinafsi mdogomdogo na hofu ambayo inaambatana na wanandoa , pia ya jinsia ya kibinadamu katika mpango wa Mungu. Papa anasema kwa hayo yote ni kwa nji ya mwanga wa kifo cha Yesu msalabani , utaweza kuelewaka upendo wa bure wa wanandoa hata kufa.Kwa Mungu ndoa siyo kipeo cha hali nzuri cha ujana , bali ni ndoto amabayo viumbe wake wataondokana na upweke ki ukweli kuna ofu katika mioyo ya binadamu  ya kujongea katika mpango huo

 

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.