2015-10-02 16:14:00

Sinodi : Kardinali Baldisseri aelezea juu ya utaratibu wa Sinodi ya Familia


Jumamosi 3 Octoba katika viwanja vya mtakatifu Petro kutakuwa na mkesha wa Sala ya kuombea  Sinodi kuhusu familia, ambapo Papa Francis ataudhuria mkesha huo akiwa pamoja na  wawakilishi,  baba wa Sinodi na wageni wasikilizaji wa Sinodi hiyo  na waumini wote kutoka pande zote za dunia.Mkesha huo uliandaliwa na Baraza la maaskofu wa Italia, waliwakaribisha familia zote,  mashirika mbambali ya kitume, vyama vya Kanisa washiriki mkesha huo.

Saa za jioni,  familia wote watapendeza wakiwa  na mishumaa  inayowaka ambapo pamoja na maombi mengine sala  ya Roho Matakatifu itaongoza   watu wote kwa mungu kwaaajili ya kuombea ya kazi itakayofanyika ya mkutano wa sinodi  kuanzia Oktoba 4-25,2015. Cardinali Baldisseri alisema ya kwamba kwenye Misa Takatifu ya kuanza Sinodi , itafanyika Jumapili Jumapili 4 Oktoba asubuhi ambapo itaadhimishwa na baba Mtakatifu Francis kwaajili ya Sinodi hiyo   ikiwa na mada  ya Wito na utume wa familia katika Kanisa na ulimwengu  mamboleo.

Sinodi hii inafanya  waaumini wa dunia  kuungana katika safari ya pamoja na wachungaji wake kupitia Mchungaji Mkuu mtakatifu Petro ( cum Petro et sub Petro)Mkutano huo unawakilisha kipindi cha mwisho cha safari ya maandalizi ya miaka 2 iliyopita  tangu walipotuma maswali kwa Kanisa lote duniani , wakitaka  wanafamilia wote duniani, wajadili kwa pamoja juu ya utajirii wake na hata changamoto zake.

 Baadaye ilifuatia Mkutano mkuu  Maalumu ambao ulifanya kazi ya kupitia majibu yaliyotolewa na waumini na kuweza kuwandika kazi ya mwisho ya Instrumentum Laboris .Kwa kazi ya maandishi , iliyojumuisha uhusiano wa Sinodi na pia  uhusiano kutoka katika madhebu mengine inawafanya sansa Mababa waajiandae kuanza kazi yao ya kusikiliza changamoto juu ya familia katika utambuzi wa wito , na wa kutangaza utume wake. Kardinali alielezea pia ratiba ya kuwa Jumamosi Oktoba 17 saa 3.00-6.30 kutakuwa na maadhimisho ya kukumbuka ya miaka 50 ya Sinodi ya maakofu, ambayo itafanyikia katika ukumbi wa Paulo VI .Mbali na washiriki wa Sinodi itakayokuwa inaendelea pia wanakaribisha wote watakaopenda kuwepo .

Kwenye  mawazo ya mwenye heri Paulo VI, ambaye aliianzisha Sinodi hiyo ya maaskofu Septemba 15, 1965, ni kwamba Sinodi  ilikuwa ni  kuendeleza roho ya Mtaguso wa Pili wa Vatican , ili  kwamba hata baada ya kumalizika ipate "kuendelea kuwafikia watu wakikristo na   wapate kunufaika kwa wingi furaha ya mkutano wa baraza la maaskofu ambao  walikuwa wamemaliza.

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.