2015-10-01 16:38:00

Papa: Furaha ya Bwana ni nguvu yetu, mioyo yetu kamwe isizimike shahuku ya Mungu


Vatican Radio: Furaha ya Bwana ni nguvu yetu ,kwani kwake yeye tunapata utambulisho ,na mioyo yetu kamwe isizimike kamwe shahuku ya Mungu. Ni mojawapo ya maneno ya Papa Francis katika misa ya asubuhi ya Alhamis 1 Octoba  katika Kanisa la Mtakatifu Marta,   Wakati Kanisa likiwa linafanya kumbukumbu ya Mtakatifu Teresa wa Mtaoto Yesu, ambaye Baba mtaktifu anapenda kumtumia mifano yake  katika mahubiri yake.

Papa Francis akihubiri kutoka katika somo la kwanza la kitabu cha Nehemia, alisema watu wa Israeli  baada ya siku nyingi za kukaa nje ya nchi yao, na sasa walirudi Yerusalem, lakini ikumbuke ya kwamba hata kama walikuwa wakiishi utumwani  huko Babilonia, daima walikumba nyumbani kwao.

Na kwa habati nzuri baada ya miaka mingi  ikawadia siku ya kurudi kwao, na  kuijenga upya Yerusalem.Neemia alimwomba mwandishi wa kale Esdra asome mbele ya watu kitabu cha sheria, na watu walifurahi sana hadi kutoa machozi maana walisikia Neno la Mungu ambalo liliwapatia furaha hadi wakalia kwa pamoja.Lakini Papa aliuliza jambo hilo linaweza kuelezwa kwa namna gani,? Majibu ya kulia si kwamba watu wamepata kurudi katika nchi yao walikozaliwa  au mji wa Bwana , bali watu hao walisikia neno hilo ambalo liliwapa utambulisho na ndiyo maana wana furahi   na kulia.

Walikuwa wamepata utambulisho  ambao kwa miaka mingi waliupoteza , japokuw katika maneno ya neemia yanasikika ya kwamba katika njia yenu  msifadhaike kwa sababu furaha ya Bwana ni nguvu yenu, na hivyo Papa alisema ni  furaha ambayoBwana uwapatia wale ambao wanapata wana mtambua.Papa alibaninsha namana ya kupoteza utambulisho na kusema,  mara nyingi utambulisho kwa Bwana  upotea katika safari nyingi za kuhamahama , na hasa tunapotengeneza viota mara hapa na pale na siyo katika nyumba ya Bwana.

Papa aliuliza ni kwa namna gani tunaweza kupata utambulisho wetu wenyewe, na hasa mtu napopoteza kile alichokuwa nacho , kama nyumba iliyokuwa yake binafsi.Papa alisema mara nyingi ni ile shahuku ya kutamani ili upate kurudi katika nyumba yako. Lakini katika somo linasema watu hao walijisikia wenye furaha na  walilia kwa furaha kwasababu hamu yao waliipata ambayo ni neema ya Mungu.

Papa alitoa mifano ya kwamaba iwapo tuna chakula cha kutosha, hatuna njaa. Kama tuna maisha mazuri tumetulia mahali tunapoishi , hatuna haja ya kwenda mahali popote.Jambo hilo linatufanya tujiulize wote “je mimi nimetulia, je ninayofuraha, sina haja ya kitu kingine kiroho, je shahuku yangu umezimika,na hasa ninapowatazama watu hao waliokuwa wakilia kwa furaha? Papa alisema moyo ambao ahauna shahuku si rahisi kutambua sikukuu,na ya kwamba safari yao waliyoanza kwa miaka mingi iliishia kwenye furaha.

Watu hao walishangilia kwa furaha kubwa kwasbabau walikuwa wametambua maneno hayo yaliyokuwa yamesomwa kwao.Walipata ile shahuku ambayo iliwafanya wajisikie kwenda mbele. Na hivyo Papa alisema tuombe kutambua shahuku tuliyo nayo kwa Mungu: na hasa kuona kama tunayo furaha, na kama kila siku tunayo shahuku ya kwenda mbele. Na mwenyezi Mungu atujalie neema hiyo na kwamwe mioyo yetu isizimike shahuku ya Mungu.

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.