2015-09-28 16:43:00

Papa Francis: Jengeni maisha yenu katika upendo maana upendo wa Mungu ni kwa kila mmoja


Jumapili 27 Septemba Papa Francis ameadhimsha kilele cha Misa Takatifu katika Uwanja wa Benjamini Franklin Parkway huko Philadelphia katika Mkutano wa dunia wa Familia kwa mwaka 2015.Mkutano wa siku mbili umeunganisha maelfu ya wajumbe kutoka sehemu mbambali za dunia ambao waliwakilisha familia za nchi zao. Na katika Homelia ya Papa Francis iliwatia moyo wanafamilia kujenga maisha yao katika upendo na kuwakumbusha kwamba upendo wa Mungu ni kwa kila mmoja  .

Akichambua juu ya masomo ya siku Papa Francis alisema: Neno la Mungu la siku linaleta mshangao na kutoa picha yenye nguvu na kuchochea sura. Sura hizo ni changamoto kwetu, lakini zinatia shahuku yetu.Kwenye somo la kwanza Joshua alimwambia Musa ya kwamba watu wawili kati yetu wanatoa unabii, wakiongea maneno ya Mungu bila kutumwa. Na katika Injili Yohane anelezea juu ya wanafunzi waliomkataza  mtu aliyekuwa anafukuza mapepo kwa jina la Yesu.  

Papa alisema kweli  huo unaleta mshangao; kwani Musa na Yesu wote wana uwezo wa kukemea. Yesu alikutana na vizingiti  kutoka kwa watu wake  ambao hawakupokea kile alichokuwa akisema na kufanya. Maneno yake yalipokelewa na watu wale walikuwa wazi na waaminifu na wa kweli katika imani ya wanaume na wanawake wengi ambao hawakuwa  sehemu yoyote  ya wateule wa Mungu.Aliongeza Papa ya kwamba wanafunzi katika sehemu yao walitenda kwa imani yao njema.

Lakini majaribu na mashaka yao yalikuwa kuhusu uhuru wa Mungu ambaye uwanyeshea mvua watu wote wanyoofu na wasio na haki (Mt 5:45), yaani wale wenye  urasimu , wenye madaraka na duru za ndani , wanaotishia ukweli wa imani na kwa hivyo ni lazima kwa nguvu kukataliwa.

Lakini Papa akabainisha ya kwamba Mara sisi tunapolitambua , tunaweza kuelewa kwanini maneno ya Yesu yalileta kashfa miongoni mwao. Ukweli wa Yesu haujali kashfa za kila kitu ambacho ujaribu kuvunja na kuharibu imani yetu katika kazi ya roho! Mapenzi ya baba  hayataisha kamwe ya  kuendelea na ukarimu wake wa kupanda .Yeye utawanya mbegu za uwepo  wake katika dunia yote , kwa maana upendo wake unasisitiza hivyo ya kwamba siyo sisi tuliyompenda Mungu bali kwamba Munga alitupenda yeye kwanza (Yn 4:10)

Upendo wake unatupqtia uhakika ya kwamba Mungu ametuchagua , na anatusubiri .Na hii ndiyo inawapa wanafunzi  wake kuhamasika , na kutoa huduma ya  kutenda mambo yaliyo mema yanayotekea kwa majirani zao wanao wazunguka. Kwani Mungua anataka watoto wake wote washiriki katika sikukuu ya Injili. Ni watu wangapi walioko pale katika madhimisho ya Familia; papa alisema: Hii peke yake ni jambo la unabii , ni aina ya miujiza katika dunia ya leo,  wote wanaweza kuwa manabii, wote wanaweza kufungulia miujiza ya upendo kwaajili ya familia zote za dunia, na hivyo kushinda kashfa nyembamba, upendo mdogo uliojifungia ndani yake yaani ubinafsi.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.