2015-09-28 14:54:00

Mkutano Mkuu wa Baraza la Umoja wa Mataifa : Marais watoa michango wao


Mkutano Mkuu wa  70 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa umeanza  rasmi Jumatatu hii 28 Septemba 2015, katika Makao  Makuu ya Umoja huo jijini New York Marekani, kwa wakuu wa nchi na serikali, kuanza  kuhutubia katika kikao hicho cha siku tatu.

Mjadala huu unaendelea  baada ya kupitishwa kwa ajenda ya maendeleo endelevu, SDGs inayoweka mwelekeo wa mustakabali wa dunia katika utendaji wa  miaka 15 ijayo.

Kwa mujibu wa ratiba, kikao kimeanza kwa hotuba ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ambaye amewasilisha taarifa ya  mwaka ya utendaji wa chombo hicho kufuatia hotuba ya  Rais wa Baraza Kuu Mogens Lykketoft aliyetoa hotuba ya ufunguzi.

Aidha wakuu wa nchi   Afrika Mashariki Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Uhuru Kenyatta wa Kenya, walitarajia kutoa hotuba zao Jumatatu hii.Viongozi wengine wa Dunia waliokwisha toa hotuba zao ni Rais Barack Hussein Obama wa Marekani ambaye amesema  mafanikio yaliyopatikana katika malengo yaliyopita ni jambo la kujivunia , lakini hata hivyo , bado kuna kazi kubwa ya kufanya. Na hivyo amesisitiza zaidi katika masuala yaliyobaki nyuma kama sekta ya afya ya umma na kuvunja mzunguko wa umaskini. Amesisitiza mataifa tajri kutoa msaada wa kutosha kwa ajili ya kuinua walio baki katika dimbwi la umaskini, kwa kuwapa nyenzo za kufanikisha maendeleo yao wenyewe. Lakini akasema, hili linawezekana tu iwapo dunia itafanyakazi kwa ushirikiano.

Na  Rais Mohamed Buhari wa Nigeria amesema ijapokuwa nchi za  Afrika hayachangii  sana katika sababu zinazoleta uharibifu wa mazingira, Afrika ndiyo inateswa zaidi na mabadiliko ya tabianchi. Na kwamba hakuna nchi inayoweza jigamba kutoathiriwa na mabadiliko ya tabianchi, hata nchi zilizonga mbele katika maendeleo kama nchi za Magaharibi, pia kuna taarifa nyingi za uharibifu unaotokana na mabadiliko ya tabia nchi .  Kiongozi huyo ameweka wazi wanacho kishuhudia  nchini Nigeria, kwamba ni  kupanda kwa joto na viwango vya usawa wa bahari, kusongea kwa jangwa, mvua nyingi, maporomoko ya ardhi na mafuriko, yote haya yakitishia mazingira. Na hivyo akasisitiza utendaji wa pamoja wa mataifa katika kukabiliana na majanga haya. 








All the contents on this site are copyrighted ©.