2015-09-28 14:28:00

Mataifa ya Afrika Mashariki yachukua tahadhari za kupambana na El Niño


Kikundi cha Ubia wa Makampuni kadhaa kwa ajili ya Maendeleo Kenya  , Benki ya Dunia na Shirika la Chakula Duniani, yamethibitisha kutenga fedha, kwa ajili ya utoaji wa msaada kwa wananchi, iwapo kutatokea  maafa ya mvua kubwa za El Niño nchini  Kenya .

Ahadi hizo zilitolewa katika mkutano uliofanyika chini ya uenyekiti wa Naibu Rais William Ruto katika makazi yake rasmi katika Karen, Nairobi hivi karibuni.  Kati ya waliohudhria ni Makatibu wa Baraza la Mawaziri, Katibu Eugene Wamalwa na Rachel Omamo , pia wakiwepo wakuu kadhaa wa mikoa na mashirika ya kimataifa. .

Akizungumza kwa niaba ya Kikundi cha Makampuni kwa ajili ya maendeleo, Bibi Julia Kronberg,  alinukuliwa akisema , kuna fedha zilizotengwa kwa ajili ya kusaidia utoaji wa msaada kwa waathirika na maafa yoyote yatakayojitokeza katika kipindi hicho.

Na msemaji wa Umoja wa Ulaya, Eric Habers alisema serikali inaweza kutumia sehemu ya fedha za msaada wa Umoja wa Ulaya ,  kiasi cha bilioni Sh3.5 zilizotengwa kwa ajili ya kukabiliana na ukame kwa El Niño.

Nayo taarifa ya Serikali, inasema ,  zinahitajika kiasi cha shilingi za Kenya bilioni Sh15.5 kukabiliana na dharura yoyote  itakayoletwa kwa  mvua  za El Niño. Hata hivyo ,  Bw Ruto aliweka wazi kwamba, hadi ni  Shilingi bilioni Sh5 tu zilizokusanywa na hivyo kuna upungufu wa Shilingi bilioni Sh10. Benki ya Dunia nayo ilisema tayari imeweka kando fedha kwa ajili ya sekta ya afya na barabara, iwapo kutakuwa na dharura zozote katika kipindi hicho.

Tanzania :Wakazi wa Mkoa wa Rukwa watahadharisha uwepo  el Nino.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Bw Saidi Magalula amewaonya wakazi wa kanda ya Kusini Magharib mwa wa Tanzania, uwepo wa tishio la mvua za El Nino na kutoa  wito kwa wananchi kuchukua hatua mwafaka ili kujikinga na maafa.

Bwana Magalula ilionya wakati akihutubia viongozi waandamizi wa serikali na halmashauri za Nkasi, Kalambo, Sumbawanga na Manispaa ya Sumbawanga, mkutano uliofanyika ofisini kwake.  Ukanda huo mara ya mwisho ulikubwa na mvuakubwa za el Nino mwaka 1997 na kusababisha maafa makubwa ikiwemo watu kupoteza maisha na mali kuharibiwa kwa wingi ikiwemo majengo, mifugo na mazao.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ametoa tahadhari hii  kulingana na halisi iliyotolewa na Mamlaka ya Utabiri wa Hali Hewa  Tanzania (TMA)  kwamba kuna uwezekano wa kuwa na mvua kubwa katika miezi ijayo.

Shirika hilo tayari limetoa onyo kwamba mvua zinatarajiwa  kuwa juu ya wastani, hivyo likaomba baadhi ya kanda kuchukua hatua mwafaka za kujiepusha na maafa. hasa katika kipindi cha October- Desemba 2015 wakati wa msimu wa mvua katika Pembe ya Afrika na kwingineko.

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.