2015-09-24 09:39:00

Hotuba ya Papa kwa Maaskofu wa Marekani


 Jumatano majira ya saa tano na nusu za Marekani, Baba Mtakatifu Francisko, alikutana na Maaskofu Katoliki wa Marekani katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Mathayo la Mjini Washington D.C.

Katika hotuba yake , alitoa shukurani zake za dhati kwa Maaskofu kwa jinsi wanavyo liongoza kanisa mahalia katika kuwa mstari wa mbele kwenye kuwahudumia watu wa Mungu  bila kujali tofauti.  Na alionya dhidi ya lugha kali na yenye kutenganisha watu kwamba huo si ulimi au  maneno yanayostahili  kutoka kwa Mchungaj. Na ndivyo ilivyo kwake pia kama Mchungaji wa Kanisa la Ulimwengu, ni lazima matendo yake na maneno yake na mwili mzima vionyeshe sura  ya Mchungaji. Hivyo  si mastahili yake kuwa na lugha mbaya yenye kutatiza na kuleta mgawanyiko kwa watu, lakini badala yake ni lazima kuwa na lugha ya kawaida na 'mkweli na lugha ya ushindan'.

Papa amewahimiza ndugu zake katika utumishi wa Kanisa, Maaskofu wa  Marekani, kusimama imara katika kutetea ulinzi wa uhuru wa dini. Aliwataka wote wawe macho katika kudumisha haki za wananchi ,  kuhifadhi na kutetea uhuru kwa kila jambo jema, si kwa kutumia vitisho lakini kupitia njia ya majadiliano  hadi maelewano. Uhuru wa dini,alisema bado ni tunu ya thamani sana kwa taifa la Marekani. 

Papa aliendelea kuwasisitiza Wakatoliki wa Marekani kujenga jamii ya ukweli na nyenye kuzingatia umoja, ili kulinda haki ya mtu  binafsi na jamii, na kukataa kila aina ya ubaguzi usio wa haki,. Na kwamba, iendelee kuwa halali kuonyesha wasiwasi kwa mambo wanayoona kwamba yako nje ya maadili ya watu wa Marekani nakufanya kazi kwa ushirikiano thabiti kuelekea ufumbuzi wa tatizo katika mtazamo wa haki na usawa.  Papa alieleza kwa kurejea katika matatizo yaliyojitokeza katika miaka ya hivi karibuni na kushindwa kwa miaka  mingi uzingatiaji wa kanuni za kulinda viumbe vilivyokabidhiwa na Mungu kwa Binadamu.

Na alisema kama Askofu wa Roma,  aliyeitwa katika utumishi huu na Mungu katika umri mkubwa,  na pia kwa ajili ya taifa hili la Marekani , kazi yake kubwa pia ni kudumisha umoja wa Kanisa zima na kuhamasisha njia ya upendo katika Makanisa yote, katika kina cha ufahamu , imani na upendo wa Kristo.  Na kwamba kwa kusoma nyuso za Maaskofu na mapenzi waliyomwonesha kama mwandamizi wa Petro, alikuwa na furaha ya kuwaambia hajisikii kama  mgeni katikati yao. Na kwamba anajua  vizuri changamoto zinazo wakakabili katika kupandikiza mbegu ya Injili katika mioyo ya watu na hasa watu wa tamaduni mbalimbali.

Papa akipita katikati ya kundi la Maaskofu wa Marekani  , kama moto uwakao ndani ya familia wenye kuwavutia wake kwa waume,  kupitia mwanga na jotojoto la upendo.   Na pia aliwataka Maaskofu kulitazama kwa makini  suala la wahamiaji , akihimiza jumuiya za Kikristo kuwa tayari kuwapokea wahamiaji, kutoogopa kuwapokea badala yake wawakaribishe kwa moyo wa upendo wa fumbo la Kristo ulio jengeka katika mioyo yao.

Baba Mtakatifu aliikamilisha siku ya Jumatano kwa kuongoza Ibada ya Misa kwa nia ya kumtaja Mwenye Heri Padre Junipero Serra kuwa Mtakatifu, Ibada itakayofanyika katika Uwanja wa Madhabahu ya Kitaifa yaliyoko katika Chuo Kikuu Katoliki cha  mjini Washington D.C








All the contents on this site are copyrighted ©.