2015-09-22 16:15:00

Serikali ya Ethiopia imezindua rasmi usafiri wa treni za umeme


Serikali ya Ethiopia imezindua rasmi usafiri wa treni za umeme zitakazowabeba abiria katika maeneo ya mijini. Treni hizo ni za kwanza kutumika katika nchi za Afrika za kusini mwa jangwa la Sahara. Treni hizo zitatumika katika mji mkuu wa nchi hiyo, Addis Ababa kwenye reli ya umbali wa kilomita 34.

Mradi huo umegharimu dola milioni 470 na umefadhiliwa kwa kiasi kikubwa na serikali ya China. Mamlaka za Ethiopia zimesema treni hizo zitafanya kazi kwa masaa 16 na zinatarajiwa kupunguza msongamano wa magari barabarani kwa asilimia kubwa. milioni moja  ya watu wanatarajiwa kutumia treni hizo kila siku na nauli inatarajiwa kuwa chini ya nusu dola kwa kila safari.

Nchi ya Ethiopia ianazidi  ikisifiwa kwa harakati za kupiga hatua kubwa za maendeleo japokuwa bado inakosolewa kwa kile kinachodaiwa kuhusu ukandamizaji wa upinzani na uhuru wa kujieleza wananchi.








All the contents on this site are copyrighted ©.