Jumapili, Baba Mtakatifu baada ya sala ya masifu ya jioni alikutana na umati mkubwa wa vijana waliokuwa wanamsubiri kwa hamu katika Kituo cha Utamaduni cha Padre Felix Varela cha mjini Havana.
Mahali hapo, Papa Francisco aliwahimiza vijana kuishi kwa matumaini wakijenga
mshikamano na mapenzi ya kukutana na wengine . Kituo hicho kilichoanzishwa mwaka
2011 na Jimbo Kuu la Havana kwa msaada wa Baraza la Kipapa kwa Utamaduni, hufundisha
masomo ya theolojia, falsafa, sosholojia, saikolojia na utawala wa biashara. Pia kuna
kumbi za mikutano, tamasha na maonyesho yanayofanywa kwa ushirikiano na wadhamini
wa tamasha la filamu la Amerika ya Kusini.
Papa baada ya kusikiliza hotuba nzuri ya Mkuu wa kituo hicho na risala ya mwanafunzi
kijana, aliyependa kumshirikisha Papa mawazo ya vijana katika matumaini yao kwa mustakabali
wa nchi yao, Papa, alijibu risala hiyo, kwa kuwahamasisha vijana , waweka hai ndoto
zao kwa kuzingatia zaidi mambo yanayolenga kujenga mshikamano , kuliko mambo yanayowatenganisha.
Papa pia alizungumzia juu ya tatizo la ajira kwa vijana na haja ya vijana kujijenga
katika utamaduni wa kukutana, na kuwataka wanafunzi kuweka mioyo yao na akili yao
wazi, badala ya kuyafungia waliyo nayo ndani yao wenyewe.
Aidha katika hotuba yake aliyokuwa ameiandaa tayari, Papa alishirikishana mawazo na
wanafunzi katika mtazamo wa kutafuta njia ya matumaini katika maisha yao, akitaja
njia tatu, kwanza, ikiwa ni kudumisha kumbukumbu ya urithi wao wa kiroho na kimaadili.
Pili, ni kusafiri pamoja katika njia ya maisha na wengine na tatu ni kuonyesha mshikamano
kwa ajili ya ustawi wa taifa kwa siku za baadaye .
Baba Mtakatifu alieleza kwamba, njia ya maisha humulikiwa na matumaini , tumaini linalotokana na imani kwa Kristo. Yesu, Mwana wa Mungu alishuka yeye mwenyewe na kuandamana nasi katika njia hii ya maisha. Na si tu hututia ujasiri sisi , lakini huandamana nasi , akiwa ametushika mkono . Mwana wa Mungu , aliyetaka kuwa kama sisi wenyewe, huandamana nasi katika Na kwa kuwa naye katika maisha yetu , tunajifunza jinsi kuona ukweli , kwa kukutana na kuwahudumia wengine na kutembea pamoja katika njia ya umoja na mshikamano.
All the contents on this site are copyrighted ©. |