2015-09-18 13:54:00

Askofu Ngalalekumtwa tena Kinara wa Baraza la TEC


Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Tanzania, limemchagua kwa mara nyingine Askofu  Tarcisio Ngalalekumtwa, Askofu wa  Jimbo la Iringa kuwa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC),hii ikiwa ni mara ya pili mfululizo baada ya kuwa katika nafasi hiyo kwa miaka mitatu  iliyopita. Aidha Baraza lilimchagua kuwa Makamu wa Rais wa TEC,  Askofu Mkuu  Beatus Kinyaiya Ofm.Cap, wa Jimbo Kuu la Dodoma. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi ya Katibu Mkuu wa TEC, kufuatia uchaguzi huo wa wiki iliyopita 4 Septemba 2015. 

Askofu Mkuu Kinyaiya anachukua nafasi ya Askofu  Severin Niwemugizi, Askofu wa Rulenge-Ngara ambaye ameachia ngazi kwa mujibu wa sheria ya TEC. Na Padre Raymond Saba , anaendelea kuwa Katibu Mkuu wa TEC, gazeti la Kiongozi limetaarifu. 








All the contents on this site are copyrighted ©.