2015-09-14 16:29:00

Papa Francis asema inabidi kujishusha katika safari ya maisha ya kikristo


Katika safari ya maisha ya kikristo ni lazima kujishusha kama alivyo fanya Yesu msalabani.

Ni maneno ya Baba Matakatifu  Francis wakati wa mahubiri ya asubuhi Jumatatu 14 septemba wakati Kanisa Katoliki nikiaadhimisha Sikukuu ya Kutukuka kwa Msalaba.Misa hiyo iliudhuriwa na Makaridinali 9 ambao kuanzia Jumatatu 14 hadi tarehe 16 Septemba watakuwa na mkutano wao.

Katika mahubiri hayo alionya ya kwamba lazima kuwa  makini na vishawishi vya dhambi viletwavyo na shetani ili kumharibu binadamu kwani Biblia inasema, nyoka  ni mwongo na ni mwenye wivu na  kwasababu ya vivu wa shetani , nyoka alaiingiza dhambi katika dunia, na ujanja wake  huo  umuharibu  binadamu maana  anakuahidi mambo mengi lakini wakati wa malipo, ni lazima kulipa sana, na pia   ni mlipaji mbaya.

Papa pia aliwakumbusha ni jinsi gani mtakatifu Paulo alikarisirika juu ya wanajumuiya wa Galatia walivyokuwa wanadanganyika , akisema nyinyi mmeitwa katika uhuru ni nani kawarubuni? Hata hivyo papa alibainisha ya kwamba  nyoka anajulikana tangu zamani na hivyo hakuwa mgeni kwao walikuwa na ufahamu kupitia historia ya  watu wa Israeli.

Papa aliendelea akitazama juu ya nyoka wa shaba ambaye alimwakilisha Yesu aliyetundikwa msalabani akisema , baada ya watu kuumwa na nyoka walipomkosea Mungu na Musa aliwambia wafanya hivyo kuotkana na maagizo ya Mungu, na ya kwamba kila aliyetazama hiyo picha ya nyoka alipona baada ya kuumwa na nyoka.

Papa alisema  hiyo ilikuwa ishara ya unabii na ahadi ambayo siyo rahisi kuitambua kama alivyomweleza Nikodemu, ya kwamba kama vile Musa alivyo amasha nyoka jangwani, ni lazima mtoto wa Binadamu aamshw hivyo ili kila aaminiye apate maisha ya uzima wa milele.

 

 Kwa hiyo nyoka ya shaba ilimwakilisha Yesu aiyetundikwa msalabani, lakini kwanini Bwana alitumia mfano ho mbaya na wa ukatili? Papa alijibu ya kwa urahisi ni kwasababu Yesu alikuja kuchukua dhambi zetu zote , na yeye akawa mwenye dhambi , bila ya  kutenda dhambi yoyote,.

Na huo ndiyo ujumbe wa Yesu katika Liturgia ya siku ya leo ya kwamba Yesu alijifanya mti na kujivisha dhambi kwaajili yetu japokuwa alikwa mungu akajinyeyekeza na kuwa mtii , hata mauti ya msalaba.

Papa alimalizia akisema kitendo cha kijifanya mwenye dhambi na kuwa kama nyoka japokuwa ni sura mbaya, ni fumbo. Na kwa hiyo  Tunapoangalia Yesu msalabani katika sanaa za michoro, ni katika hali halisi ni nyingine, kwani hali halisi ilikuwa mbaya sana , alikuwa amejaa  damu kwaajili yetu, na hiyo ndiyo njia aliyochukua ili kushusha nyoka katika uwanja wake. Lazima kuangalia msalaba na siyo  katika sanaa ya wachoraji , bali kuangalia msalaba  na kufikiria hali halisi ya wakati ule.

Vilevile ni kuangalia njia yake na Mungu aliye jinyenyekeza na kutuokoa. Hiyo ndiyo njia ya mkristo, Kama mkristo anataka kutembea katika njia ya maisha lazima ajinyenyekeze  kama alivyo fanya Yesu , ni katika njia ya kujinyeyekeza, lakini pia kuchukua unyenyekevu kama alivyo uchukua Yesu .

 Kwa sikukuu ya Kutukuka kwa Msalaba, Papa aliomba neema ya  kulia kwa upendo , kulia kwa ukarimu kutoka kwa mama Maria kwasababu ni Mungu wetu ambaye alitupenda na kututumia mtoto wake aliye jinyenyekeza na kutii mauti ili tukuombolewe.








All the contents on this site are copyrighted ©.