2015-09-14 09:21:00

Kardinali Kurt-mjumbe wa Papa katika maadhimisho ya Jubilee ya Abasia ya Mourice


Kwa barua ya Papa iliyochapishwa Julai 25, 2015 , iliyotangaza kumteua Kardinali Kurt Koch, Rais wa Baraza la Kipapa kwa Kukuza Umoja wa Kikristo, kama Mjumbe Maalum wa Baba Mtakatifu katika maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka kuhitimisha 1500 ya kuanzishwa kwa Abasia ya Mtakatifu Mourice (Switzerland), Kardinali atashiriki katika maadhimisho hayo hapo Septemba 22, 2015.

Na kwamba  Kardinali Kurt Koch ataandamana na viongozi wengine wafuatao:. Markus Bùchel, Askofu wa  Sankt Gallen na Rais wa Baraza la Maaskofu la  Uswisi, na Padre Marc de Pothuau, O.Cist., Abate wa abasia ya  Hauterive, Fribourg.

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.